Golikipa wa Manchester United, David Degea amemtaka maisha mema rafiki yake na golikipa namba tatu wa Manchester United Sergio Romero ambaye ametaarifa na klabu kuwa ataachiwa mwishoni mwa msimu huu.

Degea anaeleza kuwa anaamini Sergi Romero anahitaji kuhudumiwa vizuri aendapo na wala sio kudharauliwa kama alivyokuwa akifanyiwa pale Old Trafford.

Romero hajacheza mchezo hata mmoja msimu huu kutokana na kurejea kwa Dean Henderson ambaye amekuja kuchukua nafasi ya Degea pale United. Romero amekuwa benchi kwa muda wa msimu mmoja na ataachwa mkataba wake utakapomalizika.

ESPN waliripoti mwaka jana kuwa wachezaji wengi wa United walisikitishwa sana na suala la timu yao kushindwa kumuachia Romero aende Everton ambapo alihitajika kwa dau la pauni milioni 10 tu!

Hatimaye walimlazimisha Romero kusalia hapo kwa msimu mmoja zaidi bila ya kumpa hata mchezo mmoja wa kucheza. Baada ya siku za hivi karibuni, nafasi ya Degea pia bado haijulikani kutokana na Henderson kuwa kwenye kiwango kikubwa!

De Gea aliandika kwenye Instagram: ‘Kila la heri, Chiqui! Nakutakia kila la heri, rafiki yangu. Unahitajiwa kuheshimiwa katika changamoto yako mpya. Furahia.” Bado haijajulikana Romero ataelekea wapi baada ya kutoka OT.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa