Tetesi zinasema, Manchester United wameambiwa kuwa itawagharimu kiasi cha pauni milioni 81.5 kumsajili winga Jadon Sancho,21, kutoka Borussia Dortmund.

Tetesi zinasema, Tottenham itafanya mazungumzo zaidi na kocha wa Ajax Erik Ten Hag,51, baada ya kushindwa kufanikisha uhamisho wa Antonio Conte.

Tetesi zinasema, Duncan Ferguson, 49, amekataa kazi ya ukufunzi Real Madrid kwasababu atanaka kuwa kocha wa Everton.

West Ham wanaamini kuwa David Moyes atasaini mkataba mpya wa kudumu baada ya kufanya mazungumzo na kocha huyo ambaye amehusishwa na tetesi za kurejea Everton.

 

Moyes Kuendelea Kufundisha Akiwa Karantini.

Tetesi zinasema, mlinzi wa kulia wa Atletico Madrid Kieran Trippier,30, amewaambia wachezaji wenzake wa England yuko na mpango wa kujiunga na Manchester United msimu huu.

Barcelona wanafikiria kutoa ofa iliyoboreshwa kwa kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum,30, ambaye anajiandaa kuondoka Liverpool kwa uhamisho huru, baada ya Paris St-Germain kupoteza ofa ya awali.

Kocha mpya wa Roma Jose Mourinho anataka kumsajili mmoja kati ya walinda mlango watatu: Hugo Loloris,34, wa Tottenham, Wojciech Szczesny, 31, wa Juventus au Rui Patricio wa Wolves,33.

Tetesi zinasema, Leeds United imepewa nafasi ya kumsajili Eddie Nketiah msimu huu, Arsenal ikitaka kitita cha pauni milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 22.

Tetesi zinasema, Atletico Madrid wanatarajiwa kutoa ofa mpya kwa kiungo wa kati Rodrigo de Paul, 27, ambaye pia amekuwa akihusishwa na timu za Liverpool na AC Milan.

Leicester wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Boubakary Soumare,22, anayekipiga Lille na wameendelea kuvutiwa na Tammy Abraham ikiwa mshambuliaji huyo wa England, 23, ataondoka Chelsea msimu huu.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema, Brentford ina mpango wa kumsajili mlinzi wa kushoto Gabriel Fuentes, 24, kutoka Junior FC .

Kocha wa Lincoln City Michael Appleton, mwenye umri wa miaka 45, ndiye kipaumbele kuchukua nafasi West Brom, baada ya Waggies kusitisha mipango ya kumteua Chris Wilder.

Kocha wa Bournemouth Jonathan Woodgate, 41, yuko hatarini kutimuliwa, huku kocha wa Fulham Scott Parker 40, akiwa kwenye orodha ya wanaotakiwa kuchukua nafasi yake.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa