Delap Amwaga Wino Chelsea

Chelsea wameongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji kwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji Liam Delap kutoka Ipswitch Town.

Delap Amwaga Wino Chelsea

Ripoti zinadai kwamba usajili wa mshambuliaji huyo umegharimu kiasi cha paundi milioni 30, na mkataba aliousaini Delap utamuweka Chelsea mpaka mwisho wa msimu wa 2030/31.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 alikua akitolewa macho na Manchester United, Newcastle United na Everton, lakini uwepo wa Cole Palmer ambaye waliwahi kucheza pamoja Manchester City umemshawishi kinda huyo kujiunga na miamba hao wa Stamford bridge lakini pia ushiriki wa Chelsea kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa ukiwa kigezo mojawapo cha yeye kusaini mkataba huo na kuwabwaga United walioonesha nia nae toka awali.

Delap Amwaga Wino Chelsea

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Ripoti zinaeleza kwamba Delap alichelewa kusaini mkataba na Manchester United awali kwa madai kwamba alisubiri wamalize fainali za kombe la Europa ili endapo wangelichukua kombe hilo na kufuzu kushiriki ligi ya mabingwa basi angetia wino lakini kipigo walichokipokea kutoka kwa Spurs kikatamatisha maono hayo na kumfanya abadili njia na kujiunga na Chelsea kwani Manchester hawatoshiriki michuano yoyote ya ulaya msimu ujao.

Liam Delap ambaye amekulia kwenye academia ya Manchester City ameifungia Ipswitch Town mabao 12 kwenye michezo 37 ya ligi aliyowachezea ingawa mchango wake haukutosha kuwabakiza kwenye msimamo wa ligi kuu.

“Ninaelewa hadhi ya Chelsea na naweza kuona mwelekeo ilio nao pamoja na wachezaji hawa na kocha mkuu. Hapa patakuwa mahali bora sana kwangu kujikuza zaidi, na natumai nitafanikiwa kufanya mambo makubwa na kusaidia klabu kushinda makombe zaidi.”

Delap Amwaga Wino Chelsea

Delap amekulia kwenye mazingira ya soka akichezea timu za taifa za Uingereza kuanzia ile ya vijana chini ya miaka 16 mpaka ile ya miaka 21 ingawa bado hajafanikiwa kuvaa jezi ya timu kubwa.

Kinda huyu ambaye ni mtoto wa kiungo wa zamani wa Stoke City, Rory alifanikiwa kuwekwa kwenye tuzo za mchezaji bora chipukizi wa mwaka wa ligi ya Uingereza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.