Djokovic Afutiwa VISA yake Australia.

 

Mchezaji namba moja wa Tenisi duniani, Novak Djokovic ameshuhudia VISA yake ya kuingia nchini Australia ikifutwa mara tu baada ya kuwasili Melbourne.

 

Djokovic alishikiliwa katika uwanja wa ndege wa jiji hilo kwa saa kadhaa kabla ya vikosi vya mpakani kutangaza kuwa hajakidhi sheria za kuingia na atafukuzwa.

Inasemekana kuwa sasa amepelekwa katika hoteli ya kuzuilia watu ya serikali akisubiri kuondoka kwa ndege ya nje.

Matukio hayo yanakuja huku kukiwa na msukosuko kuhusu chanjo, Djokovic alisema alistahili kucheza katika michuano ya wazi ya Australian Open.

Djokovic hajatoa tamko lolote kuhusiana na hali yake ya chanjo , lakini mwaka jana alisema kuwa anapinga chanjo.

Katika taarifa, Jeshi la Mpakani la Australia lilisema Djokovic alishindwa kutoa ushahidi ufaao ili kukidhi mahitaji ya kuingia Australia, na visa yake imefutwa.

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amekanusha kuwa mchezaji huyo anatengwa na kusema hakuna mtu aliye juu ya sheria za nchi.

Katika mkutano na wanahabari siku ya Alhamisi, Bw Morrison alisema kuwa alishauriwa kuwa hakuna ruhusa ya matibabu kwa mchezaji huyo kuingia na kuongeza kwamba ushahidi uliotolewa hautoshi.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe