Klabu ya Barcelona inamuhitaji mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Edinson Cavani kwenye dirisha hili la Januari baada ya Juventus kuthibitisha kuwa Alvaro Morata haendi popote kwenye dirisha hili.
Baada ya kocha wa klabu ya Barcelona kushindwa kunasa saini ya Morata, sasa amehamia kwenye plan B yake ya kutaka kupata mshambuliaji ambaye ataweza kuchukua nafasi ya Kun Aguero ambaye amestaafu hivi karibuni.

Ingawa klabu ya Barcelona wana kipindi kigumu kwenye usajiri, lakini wamepanga kuweza kupunguza wachezaji wote wenye mishahara mikubwa ili kuweza kupata nafasi ya kuweza kusajiri wachezaji wapya, wachezaji ambao wamefunguliwa milango ya kuondoka ni Philippe Coutinho na Samuel Umtiti.
Ijapokuwa anahitajika na klabu ya Barcelona na muda anaopewa kucheza kwenye klabu ya Man Utd ni mdogo, lakini bado ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Man Utd na mkufunzi wa muda Ralf Rangnick ana nia ya kuweza kumbakisha kwenye kikosi chake.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


