Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Mkurugenzi wa michezo wa Lazio, Igli Tare ameanzisha mazungumzo na Liverpool kumhusu mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, huku Reds wakiwa tayari kumuuza nyota huyo wa miaka 26 kwa kuhofia kumpoteza kwa uhamisho wa bure mwezi Juni.

Tetesi zinasema, Manchester United wamedhamiria kumsajili kiungo wa Wolverhampton Wanderers na Ureno Ruben Neves, 24,mwezi huu.

Mkufunzi wa Aston Villa Steven Gerrard amempigia simu binafsi kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, ambaye alicheza naye Liverpool, kuhusu uwezekano wa Mbrazil huyo wa miaka 29 kuhamia Villa Park kwa mkopo.

 

Philippe Countinho Anaichagua Arsenal?

Liverpool huenda ikamruhusu mlinzi wa Wales Neco Williams, 20, na beki wa Muingereza Nathaniel Phillips, 24, kuondoka klabu hiyo katika dirisha la uhamisho wa Januari.

Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 31, anajiandaa kuondoka Juventus, ambako analipwa euro 325,000 kwa wiki.

Kiungo wa Everton Lucas Digne, 28, huenda akahamia klabu nyingine ya Ligi ya Primia. Hata hivyo Newcastle sio chaguo la mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Tetesi zinasema, Chelsea wanatafakari uwezekano wa kumnunua beki wa Barcelona na Marekani Sergino Dest, 21, kama mbadala wa Digne.

 

Tetesi zinasema, Newcastle wamepewa beki wa Ufaransa Samuel Umtiti 28, na Barcelona kwa mkataba wa bure na chaguo la kumnunua.

Tetesi zinasema, Borussia Dortmund watafanya uamuzi kuhusu hatma ya mshambuliaji wa Norway wa miaka 21 Erling Braut Haaland wiki chache zijazo.

Tetesi zinasema, West Ham wamewasilisha dau la pauni milioni tano kumnunua kwa mkopo mshambuiaji wa Flamengo Mbrazil Gabriel Barbosa, 25, hadi Disemba 2023.

Manchester United wanajaribu kumsajili mlinzi wa Ufaransa Dan-Axel Zagadou, 22, ambaye yuko huru kuondoka kwa uhamisho wa bila malipo kutoka Borussia Dortmund.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.