Golikipa wa AC Milan Donnarumma anaripotiwa kuwa tayari ameshawaaga wachezaji wenzake baada ya ushindi wa Atalanta dhidi ys Inter Milan.

Tuttorsport waliripoti kuwa Mino Raiola hajafurahishwa na ofa ya Milan kwa golikipa huyo yenye thamani ya €8m kwa mwaka, na yeye alitaka mteja wake kulipwa angalau €10m kwa mwaka.

Mkataba wa golikipa huyu muitaliano unafika mwisho Juni 30, 2021. Na taarifa zinasema Raiola aliomba kamisheni ya kati ya €15m na €20m.

Mustakabali wa Gianluigi Donnarumma Milan
Donnarumma

Hata hivyo, Milan wanaonekana kutokuwa na mpango kabisa wa kukubaliana na wasilisho la Raiola, na wanahisi watakuwa wanamnunua mchezaji ambaye wamechangia kumkuza vyema kwenye soka kwa gharama zaidi.

Taarifa kutoka Milan, ziripoti kuwa Donnarumma tayari alikuwa amewaaga marafiki zake na wanatimu wenzie kuwa anaondoka klabuni hapo licha ya klabu yake hii kufuzu ligi ya mabingwa kwa msimu ujao.

Kutokana na hali ya mkataba wake na sintofahamu inayoendelea katika makubaliano kati ya wakala wa mchezaji huyu na klabu yake, huenda akashindwa kusalia Milan.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa