Baada ya tetesi mbalimbali zikimuhusisha Hazard kutaka kurejea pale Stamford Bridge, kocha wa Chelsea Thomas Tuchel ametoa maoni yake kuhusu mchezaji huyo aliyetamba na Chelsea miaka ya nyuma.

Hakika mcheza kwao hutunzwa na sio kila chakula huliwa na kila mtu. Hali si shwari sana kwa Hazard pale Real Madrid toka ahamie kutoka Chelsea. Eden amekuwa akipata majeraha yasiyoisha toka afike Bernabeu na hajapata wakati mwingi wa kucheza.

Baada ya kukutana na Chelsea katika hatua ya nusu fainali ambako walipoteza mechi hiyo, Eden alionekana kutaniana na wachezaji wengi wa Chelsea na baada ya siku kadhaa Real Madrid wakatangaza kutaka kumuacha mchezaji huyo majira ya joto kwa dau la Euro milioni 43.4 tofauti ni lile dau la 103 walilotoa mwaka 2019.

Tuchel kama kocha wa Chelsea ameeleza namna ambavyo anamuona mchezaji huyo akidai kuwa ni mchezaji mzuri na hakuna kocha ambaye hatamani kuwa na mchezaji aina ya Eden.

Ni mchezaji wa viwango vya juu na muhimu kwa miaka mingi klabuni hapa na ligi hii ngumu duniani kote”, alisema Tuchel.

Akiwa na Chelsea, Hazard alijitengenezea namba nyingi sana, akicheza michezo 352, akifunga magoli 110 na kutoa pasi za magoli 110. Je, kurejea kwake pale Chelsea kutarudisha ubora wake? Ni kitu kinachosubiriwa na watu wengi sana!


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa