Dortmund Yashusha Kipigo Kizito Bellingham Aendelea Kutakata.

Klabu ya Borussia Dortmund imetoa kipigo kizito katika mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani dhidi ya klabu ya Vfb Stuttgurt cha mabao matano kwa bila mchezo ulipigwa katika dimba la Signal Iduna Park.

Dortmund walifanikiwa kushinda mchezo wao wa sita msimu huu katika ligi kuu ya Ujerumani na kufikisha alama 19 huku wakiwa nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo.dortmundKlabu hiyo ilionekana kuutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa kwani ni vijana hao wa BVB waliofanikiwa kutengeneza nafasi nyingi na kufanikiwa kupata magoli matatu kipindi cha kwanza huku magoli yakifungwa nan Jude Bellingham, Nicklas Sule, pamoja na Giovanni Reyna wakifanikiwa kuwapa BVB uongozi mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili kilianza pia kwa wenyeji kuanza msako ndipo Jude Bellingham alipoipatia klabu hiyo bao la nne kabla ya Youssoffa Moukoko kuongeza bao la tano na kukamilisha karamu ya mabao kwa wenyeji wa mchezo huo.dortmundKiungo Jude Bellingham anaendelea kuonesha ubora wa hali ya juu msimu huku tayari akiwa amefunga jumla ya mabao nane kwenye michuano yote hivo kuendelea kujiongezea thamani sokoni.

Dortmund wanaonekana kurejea kwenye makali yao baada ya kushinda michezo kadhaa mfululizo na kupata matokeo huku hali hiyo ikichagizwa na ubora waliouonesha katika mchezo wa leo dhidi ya Vfb Stuttgurt.

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.