TIMU ya Taifa ya Wasichana wa U17, Serengeti Girls imeyaaga mashindano ya kombe la dunia kishujaa baada ya kuchapwa mabao 3-0 mbele ya Colombia ambao kwa ushindi huo wamekwenda nusu fainali.

Huku Zainabu Mohamed (Dudu) aliyepewa kadi hiyo kipindi cha kwanza na kutengeneza rekodi nyingine kwa Tanzania kung’oka kombe la dunia ikiwa timu iliyopewa kadi tatu nyekundu.
Licha ya kuondolewa kwenye mashindano, benchi la ufundi la timu hiyo limeweza kufikia malengo waliyojiwekea ya kuweza angalau kufika hatua ya robo fainali kutokana na ugeni na uchanga wa kushiriki mashindano hayo.
Ikumbukwe kuwa hii ilikuwa ni mara ya kwanza Tanzania inashiriki mashindano makubwa ya FIFA na walifika hapo kwa kuwatoa vigogo Cameroo.

Serengeti ilitinga hatua ya robo fainali kwa kuwachapa Ufaranasa mabao 2-1, kutoka sare na Canada ya bao 1-1, huku wakifungwa na Japan ambao walikuwa vinara wa kundi D.
Unaweza kua kutazama video za uchambuzi na matukio ya kisoka kwa kugusa video hii

