EPL na Usajili wa Dirisha Dogo. Wachezaji Hawa Watapona?

Baadhi ya wachezaji wanataabika kwenye vikosi vyao kwa sababu mbalimbali msimu huu. EPL inawakosa baadhi ya wachezaji ambao waliwahi kuwa na sifa za kuvutia kwenye ligi hiyo.

Kuelekea usajili wa dirisha dogo mapema Januari Mosi, 2021. Baadhi ya wachezaji pengine ndio muda wao wa kutoka kwenye vifungo walivyopo kwa sasa kwenye klabu zao.

Tuwaangalie baadhi ya wachezaji wanaotabika msimu huu kwenye EPL.

  Marcos Rojo – Manchester United.

Marcos Rojo

Rojo alikuwa mchezaji muhimu kwenye safu ya ulinzi ya Timu ya Man United kabla ya maisha kumuendea kombo na alitolewa kwa mkopo msimu uliopita. Japokuwa maisha yake ndani ya klabu ya Estudientes hayakuenda sawa kutokana na mlipo wa COVID19, alirejea United na hayupo kwenye kikosi cha timu hiyo kinachocheza EPL msimu huu.

Newcastle na Sheffield United ni miongoni mwa vilabu vinavyotajwa kuhitaji saini ya Rojo kwa mkataba wa mkopo mwezi Januari. Endapo taarifa hizi zitakuwa na uhalisia, pengine hiyo itakuwa ni njia sahihi kwa mchezaji huyu ambaye bado anamkataba wa miezi 6 na United.

   Phil Jones – Man United.

Phil Jones.

Muingereza huyu ni miongoni mwa wachezaji ambao hawana namba kwenye kikosi cha United. Safu ya ulinzi chini ya Ole Gunnar Solksjaer inatawaliwa na Harry Maguire na Victor Lindelof. Uwezo wa walinzi hawa haufanani kabisa na kiwango cha Jones.

Licha ya kwamba Jones anakumbwa na majeruhi ya mara kwa mara, bado hayupo kwenye kikosi cha United msimu huu na inasemekana yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaouzwa na timu hiyo.

West Brom na Derby County ni timu zinazohusishwa na usajili wa Jones mapema mwezi Januari.

    Divok Origi – Liverpool.

Divok Origi

Bila shaka uwezo wa Origi akiwa kwenye nafasi ya kufunga goli sio wa kutilia shaka. Kwa mashabiki wa Liverpool hupenda kumuita ‘Super Sub’, hii inatokana na uwezo wake wa kuzitumia nafasi anazozipata akitokea benchi.

Safu ya ushambuliaji ya Liverpool ipo na wachezaji wenye uwezo mkubwa zaidi ya Origi. Mo Salah, Mane, Firmino na usajili wa Diogo Jota na Takumi Minamino ni dhahiri Jurgen Klopp hamuhitaji Origi kwenye kikosi chake.

Kocha wa Wolves – Nuno Espirito Santo anatajwa kama mwokozi wa Origi kutokana na kuwa na uhaba wa washambuliaji kwenye kikosi chake. Raul Jimenez bado anaendelea na matibabu na atakuwa nje ya uwanja kwa muda, hii inawapa fursa Wolves kumtizama Origi kama mbadala sahihi wa kuziba pengo hilo.

   Mesut Ozil – Arsenal.

Mesut Ozil

Japokuwa ndiye mchezaji anayepokea mshahara mrefu zaidi kwenye kikosi cha Arteta, Mesut Ozil hayupo kwenye mipango ya kocha huyo kuanzia kwenye michezo ya EPL msimu huu mpaka kwenye mashindano ya Europa.

Pengine dirisha la usajili la Januari ndio lilikuwa fursa ya Ozil kuondoka Emirate lakini mchezaji huyu amegoma kuondoka kwa mujibu wa wakala wake – Ozil ataendelea kubaki Arsenal mpaka mwishoni mwa mkataba wake.

Ni nini kitatokea kunako EPL kwenye dirisha la usajili mwezi Januari? Nani atabaki na nani ataoneshwa mlango wa kutokea? Weka maoni yako kwenye kisanduku cha maoni.

Hakika EPL kunajambo litatokea msimu huu!!!


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

17 Komentara

    Januari hapatoshi kwenye usajili bado macho kwa Mancity juu ya Messi

    Jibu

    Safi saaaana

    Jibu

    This news is very complicated

    Jibu

    Dirisha dogo la usajili patakuwa hapashikiki

    Jibu

    Msimu wa kuvunja rekod

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Hapo mambo yanazidi kunoga

    Jibu

    Msimu wa kuvuna pesa huu

    Jibu

    Imekaa powa sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Mambo n moto

    Jibu

    Hiko poa sana

    Jibu

    Januari hapatoshi kwenye usajili bado macho kwa Mancity juu ya Messi

    Jibu

    Imekaa poa

    Jibu

    Mambo hayo

    Jibu

    Wote wanauzika tu

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.