Wapenzi wa mchezo wa kikapu muda sio mrefu ile hamu ya kuuona msimu mpya wa NBA ukikatwa utepe, itakwisha. Timu mbalimbali kurejea viwanjani na kombe kugombewa upya!!
LA Lakers kufungua duru la msimu mpya wa NBA leo usiku watakapochuana na LA Clippers, huu ni mchezo utakaohitimisha historia ya kuwa na msimu mfupi zaidi wa mashindano hayo kwa msimu wa 2019/20.

Sambamba na mchezo wa ufunguzi, Lakers watakabidhiwa medali zao za dhahabu kama ilivyodesturi ya NBA – bingwa wa msimu uliopita anakabidhiwa tuzo hizo mwanzoni mwa msimu unaofuata.
Baadhi ya viwanja vitakuwa na mashabiki wakati ambapo vingine havitokuwa na mashabiki kutokana na taratibu za kujilinda na COVID19.
Tuuangalie msimu mpya wa NBA, yapi yanayojiri msimu huu?
Utawala wa LeBron James Utaendelea?

James ni ushuhuda wa mtu aliyezaliwa na kipaji chake, ulimwengu wa mchezo wa kikapu unatambua hilo. Akiwa na umri wa miaka 35, bado anatambulika kama mchezaji bora wa muda wote kwenye mchezo huo.
Alipotua LA Lakers 2018, James aliahidi makombe kumfuata na alijitahidi kulitimiza hilo na mwisho wa msimu waliibuka wababe wa NBA msimu uliopita. Sio siri, huwezi kumtaja James bila swahiba wake – Anthony Davis ambaye walikuwa wakishirikiana kufa na kupona kuhakikisha Lakers wamefika walipofika. Vipi msimu huu, James ataendelea kutawala??
Kurejea kwa Kevin Durant au muite ‘Unicorn’.

Licha ya kuwa nje ya uwanja kwa sehemu kubwa ya msimu uliopita, Kevin Durant anarejea tena uwanjani msimu huu akiwa na Brooklyn Nets.
Durant anajulikana kwa ufundi wake wa kucheza na mpira na kikapu, uwezo wake wa kupachika magoli kama mshambuliaji ni kati ya vitu vinavyomfanya Durant kuwa mshambuliaji hatari zaidi kwenye NBA.
Upinzani wa Durant vs LeBron James sio wa kitoto. Hawa jamaa wanapokutana uwanjani, mechi hiyo huwa ni ya vuta ni kuvute, ni burudani isiyokifani msimu huu.
Giannis Amelamba Mkataba Mnono Bucks. Je, ataipeperusha vyema bendera ya Bucks?

Miaka 10 iliyopita, Giannis Antetokounmpo alikuwa akiuza miwani za jua kwenye fukwe za nchi kwako – Ugiriki ili apatefedha ya kuisaidia familia yake. Wiki iliyopita, alisaini mkataba mnono ulioweka historia kwenye Ligi ya NBA baada ya kupata mkataba wa miaka 5 wenye thamani ya dola milioni 228.2
Akiwa na miaka 26 tu, Giannis anashikilia wadhifa wa kuwa MVP na Mlinzi Bora wa Mwaka kwa msimu uliopita. Milwaukee Bucks hawajabeba taji la NBA tangu 1971 na kwa uwekezaji uliofanyika kwa Giannis, ni dhahiri anatarajiwa kulipafadhila kwa kuiongoza timu hiyo kwenye ubingwa msimu huu. Hili litawezekana?
Hakika msimu huu utakuwa wa aina yake. Unadhani timu gani itaibuka kidedea msimu huu?
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???



Ernest
Cant Wait to see it, Lets go Lakers
Caroline
Kazi ipo
Hopemwaikuka
It’s going to be hotter than ever
Dorophina
Tulikuwa tunasubilia kwa hamu sana
Issa
Nba wababe tu
Mwanahamisi
Kazi ipo
Adelta
Hapo tusubiri tuone
Sarah
Kazi itakuwepo hapo
Shakila mrope
Mhh pagum hapo
aisha
Tunasubili tuone
Saupha mohamed
Mambo moto
Asia Abdy
We’re waiting
Lydia Emmanuel Magoti
Kazi hipo
David Pere
LA Lakers kufungua duru la msimu mpya wa NBA leo usiku watakapochuana na LA Clippers, huu ni mchezo utakaohitimisha historia ya kuwa na msimu mfupi zaidi wa mashindano hayo kwa msimu wa 2019/20.
Fatina mfingi
Mambo yatakuwa mazuri kwa walio jipanga
farida ahmad
NBA ni mchezo mzur Sana
Mariam mtandama
Duuuh
Tatu
Kazi ipo
warda
Bora sana