Bosi wa klabu ya Barcelona Ernesto Valverde amesalimu amri kwa meneja wa vinara wa Ligi Kuu Uingereza Manchester City bwana Pep Guardiola akimtaja kama meneja bora zaidi duniani.
Mabingwa watetezi Manchester City walizimwa ndoto yao ya kutwaa taji la Ligi ya Masbingwa Ulaya kwa sheria ya goli la ugenini kwenye mtanange wa robo fainali dhidi ya Tottenham Hotspur.
Wakati Guardiola akitupiwa baadhi ya lawama na kukosolewa na baadhi ya wadau wa soka, Ernesto Valverde yeye anaona meneja huyu ambaye pia aliwahi kuwaongoza Barcelona kutwaa ubingwa mara 2 mwaka 2009 na 2011 ndiye meneja bora duniani.
Valverde anaamini Guardiola alikuwa na uwezo wa kuwapatia City mataji matatu msimu huu, hivyo ni mwalimu mwenye mbinu zaidi duniani.
“Kwa upande wangu kocha bora ni Pep Guardiola, hapana shaka hapa. Hata kama ametolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Barcelona kwa Upande wao wana kibarua dhidi ya Liverpool kwenye nusu fainali ya michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wakiendelea kufunga hesabu ya LaLiga wanapomkaribisha Real Sociedad Jumamosi.


Povel
Habar njema