Liverpool na Manchester City wametawala tuzo za mchezaji bora wa mwaka zinazotolewa na Proffessional Footbalers’ Association -PFA, tuzo hizi hutolewa kila mwaka. Van Dijk na Raheem Sterling wakiwa na nafasi kubwa zaidi kunasa tuzo hii.
Vijana wa Liverpool, Van Dijk na Sadio Mane wameungana na Sergio Aguero, Bernando SIlva na Raheem Streling wa Manchester City kwenye nafasi sita za juu. Eden Hazard pia amekuwa mchezaji pekee kutoka nje ya klabu 2 zinazochuana kuwania taji EPL kuwa kwenye orodha hii fupi.
MO Salah, ambaye alichukua tuzo hii mwaka jana hajapata nafasi kwenye 6 bora licha ya kuchapa magoli 19 kwenye Ligi.
Kwa upande wa wanawake, Fran Kiby ambaye alitwaa tuzo hii msimu uliopita ameshindwa kuingia kwenye orodha, huenda ni kwa sababu ya changamoto ya majeraha aliyoipata msimu huu.
Wanadada wa Manchester City -Steph Houghton, Nikita Parris na Keira Walsh ni kati ya waliotajwa kwenye orodha fupi, pia Erin Cuthbert na Ji So-yun kutoka Chelsea, na Vivianne Miedema kutoka Arsenal nao wapo kwenye orodha.
Mshindi wa tuzo hizi anatarajiwa kutangazwa Jumapili, Aprili 20 kwenye hafla ya utoaji tuzo kule London.
Povel
Habar njema