Kwa mujibu wa Meneja wa Manchester United, Klabu hii haitalegeza majukumu ya pogba kwa namna ambayo yeye anataka isipokuwa maslahi ya klabu yatapewa kipaumbele. Klabu hii itamtumia vilivyo nyota huyu kwa maslahi ya klabu.
Toka pogba aliporejea klabuni hapo akitokea Juventus kwa dau la paundi milioni 89 mwaka 2016, klabu hii imekuwa ikipanga namna bora ya kumtumia staa huyu kwa maslahi ya timu.
Kiwango cha Pogba kiliathiriwa na uhusiano wake uliozorota na aliyekuwa meneja wa klabu hiyo bwana Jose Mourinho katika siku zake za mwisho kabla ya kutimuliwa klabuni hapo.
Hata hivyo, kurejea kwa mchezaji wa zamani Ole Gunnar Solskjaer kama meneja kumesaidia kumrudisha mchezoni staa huyu na wachezaji wenzake. Siku chache zilizopita kulikuwa na minong’ono iliyomuhusisha nyota huyu na klabu ya Real Madrid baada nyota huyu kutaja Real Madrid kama klabu ya ndoto za wachezaji wengi wakubwa bila kujiweka kando yeye.

Meneja Ole Gunnar anasema kuwa anatambua staa huyu ni mmoja wa mastaa wenye vipaji na uwezo wa pekee katika nafasi yake, pia anaweza kubadilika badilika kwa kucheza nafasi tofauti uwanjani.
Gunnar anasema ni mpango wa klabu kuhakikisha staa huyu anatumiwa vilivyo kwa maslahi ya klabu yake ya Man United. Klabu itakuwa inafikiria kumpangia majukumu tofauti kulingana na uwezo wake na mahitaji ya michezo husika.
Pogba anatajwa kuwa na uwezo wa kucheza namba 6 au 10, ana uwezo wa kubadilika badilika kucheza kama kiungo, kusaidia safu ya ulinzi au kucheza kama mshambuliaji.
United watendelea kumtumia staa huyu kadri ya mahitaji ya klabu licha ya kuhusishwa kwake na klabu kadhaa. Kama gemu itamuhitaji aegemee safu ya ulinzi au kiungo basi atafanya hivyo, kama gemu itamuhitaji apandishe mbele basi atahitajika kufanya hivyo. Ila Pogba ni balaa!


Issa
Pogba fundi sana uwanjani