Clarence Seedorf anasema Zidane anapaswa kufanya kila namna kurejesha njaa ya mataji klabuni Real Madrid. Bila shaka njaa ya ubingwa itarejea!
Madrid walifanikiwa kumrejesha meneja Zinedine Zidane kama meneja, kocha mkuu baada ya kushindwa kufanya vyema wakiwa na Julen Loptegui na Santiago Solari na msimu ukiwaendea vibaya tofauti kabisa na matarajio yao.
Legendaeri huyu, Zidane aliipeleka Real Madrid kutwaa ubingwa mara 3 mfululizo na kutwaa taji la La Liga mwaka 2016-17 kabla hajaamua kustaafu msimu uliopita. Liverpool walishuudia kichapo kabla Zidane hajasepa Real Madrid.
Seedorf anaamini wachezaji wanahitaji kubadilishwa mitazamo yao na Zidane anapaswa atafute mbinu za kuwarejesha mchezoni wachezaji wake.
Toka amerejea tena kama meneja klabu hiyo imepoteza gemu 1 tu katika 5 ambazo Zidane amezisimamia. Lakini, wachezaji wanaonekana bado hawana ari kubwa kurejea kwenye nafasi yao ya awali.
Bila shaka kwa usoefu alionao Zidane kwa LA Liga na klabu hiyo, anaweza kuamsha tena ari ya wachezaji klabuni hapo.


Furahav
Zidane anajua.