Eto'o Alikuwa na Sababu Juu ya Balotelli

Kila mtu huwa na mtazamo yake pindi likitajwa jina la mchezaji nyota wa Italia, Mario Balotelli. Wapo wanaomuona kama muhuni mmoja tu asiyejua hili wala kutambua lile hususani katika soka. Wengine wanaona kama Balotelli ni mchezaji mzuri ambaye anasumbuliwa na ‘utukutu’ tu. Yote kwa yote, umpende ama umchukie, Balloteli ni moja kati ya wachezaji wazuri kuwahi kutokea.

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon na klabu za Barcelona na Chelsea amewahi kunukuliwa katika mahojiano na gazeti la Gazzetta Dello Sport akisema kuwa anachokifanya Mario uwanjani hakifikii hata asilimia 10 ya uwezo wake halisia!

Kauli hiyo ilipokelewa kwa hisia tofauti tofauti na wadau na mashabiki wa soka. Wapo walioibeza na wengine wakaiona kuwa ilileta maana. Siku zikaenda, miaka ikakatika, kauli hiyo ikasahaulika kwa mashabiki hao wa soka kama haikuwahi kutamkwa. Mimi ni mmoja kati ya wachache tulioguswa na kauli ile.

Ni ukweli usiopingika kuwa jina la Balotelli ni kubwa kuliko yale anayoyafanya uwanjani. Ukubwa wa jina hilo muongoni mwa mashabiki wa soka unachagizwa zaidi na vituko vya Mario ndani na nje ya uwanja. Jina Balotelli linaambatanishwa sana na sifa ya ‘utukutu’ kiasi kwamba likitajwa jina lake ni kama mtu ametaja maana nyingine ya neno utukutu!  Yamkini hii ndiyo sababu iliyofanya kauli ya Etoo ipuuzwe na isipewe uzito unaostahili.

Watu wengi wanamtambua Mario kwa matukio yake ya nje ya uwanja kama lile alilolifanya mwaka 2010 akiwa Italia pale alipoingiza gari lake ndani ya geti la gereza la wanawake na alipoulizwa alichokihitaji alisema kuwa alikua akizunguka zunguka tu!

Wengine wanamtambua kwa tukio lake alilolifanya mwaka 2012 akiwa mchezaji wa Manchester City. Ilikuwa hivi, Balotelli alikuwa kwenye mizunguko yake ya kawaida ndani ya gari lake la kifahari aina ya ‘Bentley’, lakini ghalfa akapaki gari hilo nje ya shule ya Xaverian ili tu aweze kutumia choo cha shule hiyo.

Tukio lingine la Balotelli linalokumbukwa sana ni lile alilolifanya mwaka 2009 kwa kwenda katika maojiano ya kituo kimoja cha televisheni huku akiwa amevaa fulana ya AC Milan yenye jina lake mgongoni huku yeye akiwa mchezaji wa Inter Milan! Yani ni sawa na leo hii,  licha ya upinzani wa jadi uliopo, mchezaji mmoja wa Simba afanye mahojiano na kituo cha TV akiwa amevaa jezi ya Yanga, Au wa Yanga avae ya Simba!

Kuna kipindi timu ya taifa ya Italia ilianza kutumia jezi mpya, katika hali ya kustaajabisha Balotelli alirudi kipindi cha pili akiwa amevaa jezi za zamani kwa madai kuwa hajapenda muundo wa jezi mpya!

Balotelli  hajawahi kuishiwa vituko. Anaishi kwenye ulimwengu wa peke yake. Alishawahi kufunga goli kwa shuti kali kutokea mbali kabisa karibu na duara la katikati ya uwanja, wakati wachezaji wenzake na uwanja mzima ukilipuka kwa shangwe na kushangilia yeye alikua akitembea tu taratibu kama hakijatokea kitu vile! Kuna mtu alishawahi kusema kuwa ‘huyu (Balotelli) kichwani kwake kuna sehemu umeme hauingii vizuri’ ilikua bado kidogo tu nimuunge mkono kabla sijagutuka haraka kuwa kichwa cha binadamu hakitumii umeme.

Mara kadhaa amewahi kuripotiwa kugombana na wachezaji wenzake kama Kompany, Carlos Tevez na Boateng.

Huyo ndiyo Balotelli ambaye wengi wanamfahamu, na hiyo ndiyo taswira ambayo wengi wanaiona kwake. Etoo hakuiona hiyo, na pia alitaka watu waone zaidi ya hapo.

Etoo alitaka watu wakione kile kilichopo ndani ya Balloteli uwanjani, tofauti na namna  watu walivyokuwa wanapata picha ya ‘utukutu’ likitajwa jina Balotelli, yeye alitaka ijengeke ile taswira ya mchezaji mwenye kasi, asiyechoka, mbunifu, mwenye maguvu na jicho linaloona lango! Tumuone Balotelli yule ambaye anaweza kufunga hata kwa kichwa au miguu, ama kiungo chochote cha mwili kinachoruhusiwa! Zaidi ya yote Etoo alitaka, hata pamoja na hayo tujue kabisa kuwa hiyo haifikii hata asilimia 10 ya uwezo wa Balotelli. Tusijisahaulishe. Etoo amecheza na Balotelli wakiwa wote pale Inter, anamjua vizuri zaidi kuliko sie. Sisi ni nani hata tupinge?

Kila mtu huwa na mtazamo yake pindi likitajwa jina la mchezaji nyota wa Italia, Mario Balotelli. Wapo wanaomuona kama muhuni mmoja tu asiyejua hili wala kutambua lile hususani katika soka. Wengine wanaona kama Balotelli ni mchezaji mzuri ambaye anasumbuliwa na ‘utukutu' tu.

 

Tungekubaliana na Etoo kama tungeweka hisia hasi pembeni na kuaangazi mazuri ya ‘Super Mario’.

Tusijisahaulishe mashindano ya Euro mwaka 2012, mashindano hayo yalikuwa na timu tishio sana mojawapo ikiwa Ujerumani! Sasa waulize hao Ujerumani kiliwakuta nini walipokutana na Italia katika hatua ya nusu fainali. Ukitaka wakuelewe vizuri waulize kilitokea nini walipokutana na Balotelli. Wanakumbuka vizuri kabisa kiwa aliwafunga magoli mawili mujarabu kabisa katika mechi hiyo! Wakianza kukuhadithia goli la kwanza waambie waachane nalo wakusimulie lile la pili badala yake.

Watakusimulia namna ambavyo bado hawakuwahi kuamini kilichotokea mpaka kesho. Balotelli alipokea pasi ndefu kutoka kwa Montolivo, akauvunja ukuta wa timu ya taifa ya Ujerumani nao ukatii amri hiyo bila shari, kisha akaachia shuti kali lililoenda kuzama katika kona ya kulia na lango la Ujerumani na kumuacha mlinda lango Manuel Neuer asijue la kufanya.

Etoo alitaka tumuone Mario Balotelli mwenye rekodi ya kufunga jumla ya magoli 20 katika michezo 59 aliyocheza akiwa na Inter Milan, akafunga mengine 28 katika michezo 54 pale Uingereza akiwa na Manchester City! Balotelli aliyewafungia Nice magoli 33 katika michezo 61, Samuel Etoo ‘Phills’ alitaka tumuone Balotelli kwa mazuri hayo na mengine mengi. Halafu tukishayatambua yote hayo tukumbuke kwamna bado hayo ni 10% tu ya uwezo wake wote, nadhani baada ya hapo watu wangempa Balotelli heshima anayostahili.

Lakini sasa hiyo asilimia 90 iliyobaki tutaiona vipi?  Ni wazi kuwa Balotelli anatakiwa kufanya kazi ya ziada ili tulione hilo. Asitegemee vitu kutokea ikiwa hafanyi chochote, lazima aongeze bidii. Na sisi tufanyeje katika hilo? Tumpe muda? Tunaweza kumpa muda kama tukikata, miaka mitatu au minne hata mitano, shida ni kama muda huo upo tayari kwenda kwa Balotelli! Jamaa mpaka sasa ana miaka 29, mwezi wa nane mwaka huu atatimiza miaka 30. Sidhani kama huo muda wenyewe upo wa kutosha.

44 Komentara

    Thnks meridian bet kwa habar za Kimichezo na burudani

    Jibu

    Asanteni meridian kwa michezo na burudani

    Jibu

    Jamaa napendaga mambo yake tu

    Jibu

    Good news 👍 @ # meridianBetTZ

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Alimona no mxhezaji mzuri lakini nidhamu mbovu

    Jibu

    Nguli wasoka mtukutu na style zake nyingi namkubali sana #Meridianbettz

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri Ila nimkorofi sana

    Jibu

    Yuko vizuri ila kwenye uchezaji ila tabia yake mbaya

    Jibu

    Utukutu umechangia kushuka kwa kiwango cha Mario balotelli #meridianbettz

    Jibu

    Utukutu umechangia kushuka daraja Balotelli

    Jibu

    asante meridianbet kwa habar

    Jibu

    Kwa uchezaji wake tumpe sifa zake tu

    Jibu

    Alikuwa mchezaji mzuri sana enzi hizo sena utukutu ulimzidi alafu mwenyewe alikuwa anaona ni kawaida tu hakuwa anajali kitu

    Jibu

    Balottel akaze sana,maana nidhamu sifuri

    Jibu

    Balottel..!alikua mchezaji mzuri sana..!

    Jibu

    Baloteli ni mchezaji mzuri sana,hivo hongera kwake

    Jibu

    Hahaha mimi naikumbuka tu “why always me” ila ballotel ni bonge la mchezaji ambae hajafaidi kiwango chake

    Jibu

    ahsanteni meridian kwa taarifa

    Jibu

    Ahsante meridian kwa taarifa zenu #meridianbettz

    Jibu

    Nimchezaji mzuri apunguze utukutu

    Jibu

    balotel ni mchezaji mzuli sana

    Jibu

    Baloteli ni mmoja wa mchezaji mzuri.. #meridianbettz

    Jibu

    Balloteli ni bonge la player mwenye character za kisanii yan kila nyakati anataka azungumziwe tu

    Jibu

    Nakubali Sana hyu mtu mweus

    Jibu

    Asante meridianbet kwa taarifa mahili.

    Jibu

    Mtu mtukutu anaye sakata kabumbu haatari #meridianbettz

    Jibu

    Asante sn meridianbet kwa habari mulwa za michezo Safi sn

    Jibu

    Asanten kwatarifa meridianbet

    Jibu

    tatizo la ballotel ni mkorofi

    Jibu

    tatizo lake balloten ni mkorofi

    Jibu

    Ballotel namkubali sana ajitahidi kukaza

    Jibu

    Asanteni kwatarifa meridianbet

    Jibu

    Nimchezaji nzuri mbabe wao

    Jibu

    Ahsant sana meridian kwa burudani zuri

    Jibu

    Story ya balotel hainishi hamu kuisoma

    Jibu

    Asante meridianbet kwa kutujali wateja wenu

    Jibu

    Mnatupatia tunachostahili meridian kwa habari za michezo

    Jibu

    Kwangu bado Mario Baloteli ni mchezaji mzuri na endapo ataendelea kupata nafasi ataonyesha makubwa. Bonge la makala #Meridianbettz

    Jibu

    Hajitambui yuko km msukule.

    Jibu

    Balloteli ni mchezaji mwenye kujitambua sana

    Jibu

    Da kweli alikuwa mchezaji mtata sana

    Jibu

    Jamaa anajua ila ukorof Ndio tatizo

    Jibu

    Etoo ni hatari

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.