Ferguson Asaini Mkataba Mpya na Brighton Hadi 2029

Mshambuliaji wa Ireland Evan Ferguson amesaini mkataba mpya wa miaka sita na Brighton.

 

Ferguson Asaini Mkataba Mpya na Brighton Hadi 2029

Ferguson mwenye miaka 19, alijiunga na Seagulls kutoka klabu ya utotoni ya Bohemians mnamo Januari 2021 na tangu wakati huo amefunga mabao 15 katika mechi 43 alizocheza Pwani ya Kusini.

Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Kocha mkuu Roberto De Zerbi alisema Evan anastahili mkataba huu mpya na ana mustakabali mkubwa sana mbele yake.

Ferguson Asaini Mkataba Mpya na Brighton Hadi 2029

Naye Mkurugenzi wa ufundi David Weir aliongeza kuwa Evan ni kijana mwenye kipaji na wanafuraha kwa ajili yake.

Ameonyesha uwezo wake katika ngazi ya klabu na kimataifa baada ya kuingia kwenye timu mwanzoni mwa mwaka na wanatazamia kufanya kazi naye na kutazama maendeleo yake.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Ferguson Asaini Mkataba Mpya na Brighton Hadi 2029

Ferguson alicheza mechi yake ya kwanza kwa Seagulls dhidi ya Cardiff kwenye Kombe la Carabao mnamo Agosti 2021 kabla ya kucheza mechi yake ya Ligi Kuu dhidi ya Burnley mnamo Februari 2022.

Bao lake la kwanza katika ligi kuu ya Uingereza lilifuatia dhidi ya Arsenal katika mkesha wa mwaka mpya.

Mshambuliaji wa kati wa Brighton ameendeleza kiwango chake cha kufurahisha msimu huu, akifunga hat-trick yake ya kwanza kwenye kikosi cha Amex dhidi ya Newcastle mnamo Septemba. Evan Ferguson ana mabao matano katika mechi 14 hadi sasa msimu huu.

Ferguson Asaini Mkataba Mpya na Brighton Hadi 2029

Akizungumza baada ya mchezo huo dhidi ya Magpies, De Zerbi alisema kuhusu kipaji chake changa: “Maboresho yake ni muhimu kwake, kwetu, kwa kazi yake kwa sababu anafanya kazi ili kukamilisha sifa zake, sio tu kufunga, kwa sababu anaweza kuwa mkubwa.”

Sifa zake zinatosha kuwa mchezaji bora, mmoja wa wafungaji bora barani Ulaya. Amezaliwa 2004. Sijui ni wachezaji wangapi wachanga kama Evan walifunga mabao hayo katika maisha yao ya soka. Alisema De Zerbi.

De Zerbi atakuwa na matumaini ya kuwa na Ferguson katika mchezo wa kesho dhidi ya Sheffield United, kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Ajax kwenye Ligi ya Europa Alhamisi usiku.

Ferguson Asaini Mkataba Mpya na Brighton Hadi 2029

Aliingia akitokea benchi katika ushindi wa Amsterdam na anasubiri bao lake la kwanza katika mashindano ya Uropa. Lakini kijana huyo amefunga mara tatu katika mechi nane za kimataifa.

Acha ujumbe