FIFA Imeahirisha Women's Under-17 World Cup!

Ile michuano ya wanawake imeahirishwa mpaka mwaka 2021, naam, ni ile ya women’s Under-17 World Cup ambayo ilipangwa kufanyikia India mwezi Novemba mwaka huu, kwa sasa imesogezwa mbele kwa miezi mitatu, FIFA walisema hayo siku ya Jumanne.

Hii inakuwa pigo lingine kwa wapenda michezo baada ya michezo mingi duniani kusimamishwa kwa muda.

Michuano, iliyopangwa kufanyika katika majiji matano, kwa sasa itaanza mnamo mwezi Februari ifikapo tarehe 17, bodi ya michezo inayoongoza mashindano hayo iliweka wazi suala hilo.

India inatarajiwa kuongeza umaarufu wake kimataifa kwa kuwa wenyeji wa michuano hiyo na imekuwa hivyo mara baada ya kusimamia michuano ya Under-17 World Cup mwaka 2017 kwa upande wa wanaume.

“Waandaaji wote katika majiji yaliyopangwa wameweka juhudi zao na kuelekeza nguvu zao zote mpaka sasa katika kuhakikisha mambo yanakuwa sawa kabisa, nasi tunayo furaha kwani tarehe mpya zilizotajwa zitawapa nafasi wao kujiandaa vyema zaidi kwa muda walioupoteza mwanzoni na kusonga mbele zaidi.” Kamati ya ndani ya uandaaji wa mashindano hayo ilisema hayo mara baada ya tangazo hilo la FIFA.

Pia, FIFA wameweka wazi juu ya tarehe mpya za michuano ya mwaka huu ya U-20 Women’s World Cup inayofanyika kule Costa Rica na Panama. Kwa sasa itachezwa ifikapo mwezi Januari tarehe 20 mpaka mwezi Februari tarehe 6, 2021.

Na kwa upande mwingine tena michuano ya mwaka 2020 FIFA Futsal World Cup iliyopangwa kufanyikia huko Lithuania imesogezwa mpaka mwezi Septemba tarehe 12 mwakani.

Kwa wakati huu, mkutano wa 70 wa FIFA ambao ulitakiwa kufanyika nchini Addis Ababa utafanyika kwa njia ya mtandao ifikapo mwezi Septemba tarehe 18 mwaka huu.

Michezo mingi duniani imesimama kwa muda kutokana na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Corona na kuathiri michezo mingi duniani ingawa mingine inachezwa bila ya uwepo wa mashabiki.

Kuna ligi ya South Korea iitwayo K-League imerudi Ijumaa iliyopita na ligi ya Ujerumani, Bundesliga inarejea hewani leo hii bila ya uwepo wa mashabiki viwanjani.

23 Komentara

    Ni wazo zuri kusogeza mbele kutokana na hali halisi iliyopo duniani

    Jibu

    Ni vizuri maana hali ya ugonjww wa corona bado aujakaa sawa

    Jibu

    Asante meridianbet mko vzur kwa habar za kijanja

    Jibu

    dah hii lig inakuwa na magoli sana meridianbet pesa nje nje

    Jibu

    Mwaka 2021 kutakuwa na mashindano mengi sana

    Jibu

    Ni vizuri vigezo na masharti vizingatiwe..!juu ya ugonjwa huu

    Jibu

    Sio mbaya kama iko kwenye utaratibu maalum na viongozi wanalifwatilia hilo ,hali itakapokuwa shwari mambo yataendelea.

    Jibu

    Dhaa Corona imeharibu michezo mingi lkn Ni vizuri kuepuka maambukizi ya corona

    Jibu

    Ya ni maamuzi mazuri kusogeza mbele mashindano u17 ya wanawake.! safi kwa habari moto moto za michezo# meridianbettz.

    Jibu

    Pole sana kwao kwa kukosa.mashindano yao ya msingi kabisa ya ukuaji wao wa kisoka kimataifa

    Jibu

    Asante meridian kwa taarifa za Kimichezo za Moto moto

    Jibu

    Mm nilikuwa sijui asanten meridian kwa habari Kama hizi

    Jibu

    tukaze moyo mambo yakikaa sawa mchuano utaendelea

    Jibu

    Corona ni janga la Dunia nzima, hakika tunahitaji kupambana nalo kwa kila mbinu.

    Jibu

    Afya muhimu,mashabiki tuendelee kusubr Hadi Hali itakapokaa sawa..

    Jibu

    Corona imevuruga mambo.

    Jibu

    Hali bado aiko shwar so ni vzur tu

    Jibu

    Mungu atusaidie janga lipite

    Jibu

    tuombee mungu hili janga liishe na mambo mengine yaendelee

    Jibu

    Daaah! Sio mbaya japo nayo n ligi ambayo inaburudisha

    Jibu

    Wamefanya maamuzi mema maana hali bado haijatulia

    Jibu

    wamefanya maamuzi dhabiti

    Jibu

    Duuuuh Corona siyo poa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.