Flick -  Itakuwa Maalumu Alaba Kumalizia Soka Lake Akiwa Bayern.

David Alaba bado hajakubali kuongeza mkataba na Bayern Munich, lakini kocha Hansi Flick amesema itakuwa maalumu kama atamaliza kucheza soka lake akiwa Allianz Arena.

Dili ya Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka nchini Australia inakaribia kuisha kunako klabu ya Bayern Munich na vilabu vilivyoonesha nia ya kutaka kumsajili mlinzi huyo ni PSG, Barcelona,Chelsea na Manchester City.

Kufuatia ushindi wa 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen siku ya Jumamosi, Bayern walifanikiwa kutwaa ubingwa wa  DFB-Pokal. Alaba ndiyo alianza kufunga katika fainali hiyo , Flick amesema alikuwa na nia ya kumpa mkataba mwingine Alaba mwenye umri wa miaka 28 na Thiago Alcantara.

Walakini, bosi huyo wa Bayern Munich alieleza kwamba “itakuwa ngumu” kumbakisha Thiago ambaye amekuwa akihusishwa  kuhamia klabu ya Liverpool ambao ni Mabingwa wapya wa EPL.

“Nitasimama kuhakikisha nafanya kila kitu kuwabakisha katika timu wachezaji hawa wawili wenye vipaji vikubwa,” alisema Flick.

“David amekuwa ni mchezaji wa kipekee hapa klabuni, sio tuu uwanjani bali amekuwa ni mzuri kwetu sisi.

“Anajua kuwa anakubalika sana katika klabu.Itakuwa muhimu sana kama atamalizia soka lake hapa akiwa nasi.”

53 Komentara

    Alaba anapaswa kulitilia umakini hili Bayern imemkubali sana

    Jibu

    Alaba ni mmoja ya wachez waliofany mapinduz makubw Sana Allianz ARENA Kama hata salia itakuwah Jambo kubwa sana kwa club thnks meridian kwa update

    Jibu

    Itakuwa poa sana.aongeze bidii tu

    Jibu

    Ni jambo la kutia moyo unapoendelea kuthaminiwa na kuhitajika na Klabu unayoitumikia. Inawezekana Alaba anataka kupata changamoto nyingine mahali pengine#meridianbettz

    Jibu

    Wachezaji

    Jibu

    Alaba namkubali sana,beki kisiki anatakiwa kutulia hapo.

    Jibu

    Wachezaji mahiri kama hawa huwa awawezi kubakia katika vilabu vilivyowakuza na huitaji kucheza kwingine kwa sababu ya umahiri wao na kujiongezea kipato

    Jibu

    Jambo zur na la kupendeza alaba akimaliza maisha yake ya soka akiwa munich n mpambanaji sana

    Jibu

    Bola abaki t maan ndo upepo wake wa mafanikio nd ulipo

    Jibu

    Upepo wake wamafanikio ndio ulipo

    Jibu

    ni muda kutafuta challenge mpya sasa

    Jibu

    Hana weza tu na nisawa coz sijaona timu ya kufanana nae

    Jibu

    Ni beki mzuri sana amekubalika

    Jibu

    Alamba ni kifaa ila alitakiwa aende sehemu nyingine ili kupata uzoefu zaidi ,pamoja na timu yake kumkubali .

    Jibu

    Fundi wa mpira safii sana

    Jibu

    Maoni:Bora abaki tu

    Jibu

    David Alaba ni mchezaji mzuri sana ila tatizo maslahi ndo shida

    Jibu

    Mimi naona anaweza kwenda kwingine kwenye klabu kubwa kujiwekea historia zaidi katika soka lake kwani keshaweka jina pale Bayern na bado anauwezo wa kucheza popote

    Jibu

    Tangu nimjue Huyo jamaa had Leo bado yupo hapo hapo tu angefanya mpango akamalizie career yake ya mpira club nyingine.

    Jibu

    Jamaa anajitaidi sana

    Jibu

    Ni beki mzuri Sana

    Jibu

    Bora asiondoke watamkosa mchezaji makini abaki

    Jibu

    Itakuwa vzr Sana yapasa aongezee bidii

    Jibu

    Alana ni mchezaji mzuri Sana kwa wakati huu so sioni Kama Kuna ulazima wa kumaliza soka lake pale Baryen maana siku hizi wachezaji wazuri Wana windwa na vilabu vyennye mkwanja mkubwa Kama vile Man U, PSG na nyinginezo

    Jibu

    Ni jambo la kupendeza kuona kuwa alaba anathaminiwa na klabu yake

    Jibu

    Ni vyema akimaliza muda wake apo

    Jibu

    Sio Lazima Jamani wasimfosi#Meridianbettz

    Jibu

    Maoni:nibeki bora sana

    Jibu

    Akaangalie upepo sehemu nyingine

    Jibu

    Asante kwataharifa

    Jibu

    Asaini tu huo mkataba amalize muda wake apoapo

    Jibu

    Cha msingi aongeze bidii

    Jibu

    Hitakua vizuri kwa upande wenu lakini hayo ni maamuzi yao na maslayi yao mwenyew kubaki hau kuondoka

    Jibu

    Amalize tu soka lake hapo hapo ni beki mahiri sana

    Jibu

    Ni beki mahili sana napia namkubali sana

    Jibu

    David amekuwa ni mchezaji pekee hapo kilabuni

    Jibu

    Sio lazima wasimfosi

    Jibu

    Itakuwa vizuri aongeze juudi

    Jibu

    Ni vizuri akabadilisha klabu nyingine ilikujua city vingine zaidi#meridianbett

    Jibu

    Itapendeza

    Jibu

    Itakuwa pouwa sana

    Jibu

    Fundi huyo safii sana

    Jibu

    Itakuwa uwamuzi mzuri sana maana nimchezaji tegemezi kwa baryen

    Jibu

    David amekuwa ni mchezaji wa kipekee hapa klabuni, sio tuu uwanjani bali amekuwa ni mzuri kwetu sisi mashabiki zake

    Jibu

    Inapendeza

    Jibu

    Mchezaji mzuri sana akiwa na mpira

    Jibu

    Ni beki mzuri ni Bora akabaki

    Jibu

    Vizuri kubaki bayern

    Jibu

    Nice update 👍

    Jibu

    Maoni:meridian mko vizuri kwa taarifa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.