Baada ya kuhusishwa na vilabu kadha wa kadha, hatimaye Dominic Szoboszlai ameichagua RB Leipzig na sasa anatimkia Bundesliga.
Arsenal, AC Millan na Real Madrid ni miongoni mwa vilabu vilivyohusishwa zaidi na sahihi ya Szoboszlai ambaye anakipiga katika klabu ya RB Salzburg.
Hii ni habari mbaya zaidi kwa Arsenal ambao walimtizama Dominic Szoboszlai kama mbadala sahihi wa Houssem Aouar ambaye walimkosa majira ya kiangazi.

RB Leipzig wameipata sahihi ya Szoboszlai kwa kulipa pauni milioni 18 ikiwa ni dau tofauti na ambalo vilabu vingine vilitakiwa kulipa (pauni milioni 23).
Kwa Mikel Arteta hili ni pigo kutokana na uhalisia kwamba timu yake haina mchezaji mwenye haiba ya Szoboszlai kwa sasa na wanapata tabu sana katika safu yao ya kiungo mchezeshaji. Ni Mesut Ozil pekee mwenye uwezo wa kutibu tatizo hilo lakini hayupo kwenye mipango ya kocha huyo msimu huu.
BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!



Adelta
Hii ni habari mbaya kwa kikosi Cha Arsenal
Hopemwaikuka
Kapambane tu
Rahma
Habari njema
Sarah
Duu
Dorophina
Habari njema kwa mashabiki wa rb leipzig
Issa
Rb imepata mtu
Janeflora malisa
Safi
Lydia Emmanuel Magoti
Safiii sana
Saupha mohamed
Good
warda
hongera yake
Tatu
Popote kambi
samiah
Kambi popote