Kocha wa klabu ya Fc Bayern Munich Julian Nagelsmann amesisitiza kua anahitaji klabu hiyo isajili golikipa katika dirisha dogo la mwezi Januari ambalo ndo limefunguliwa hivi karibuni.

Klabu ya Fc Bayern Munich ipo kwenye wakati mgumu kuelekea ugwe ya pili ya msimu kwani klabu hiyo inamkosa golikipa wake namba moja ambaye anasumbuliwa na majeraha. Manuel Neuer amefanyiwa upasyaji na hatakuepo mpaka mwisho wa msimu huu.nagelsmanKocha wa klabu hiyo Nagelsman anaona wanahitaji kusajili golikipa kwenye kipindi hichi cha majira ya baridi bila kuangalia golikipa huyo atakuja kuanza au taanzia nje. Kocha huyo anapiga hesabu kama golikipa wake namba mbili kwasasa Sven Ulreich akipata majeraha watapitia kipindi kigumu mno.

Kocha huyo anasema soko la usajili kipindi hichi cha Januari ni gumu haswa kwenye upande wa kutafuta golikipa, Lakini kocha huyo anasema klabu yake inahitaji kufanya namna yeyote kuhakikisha wanapata golikipa mwingine ambaye atakuja kusaidiana na Sven Ulreich.nagelsmanKocha Nagelsmann pia amzungumzia kuhusu golikipa wa Borussia Monchengladbach Yann Sommer na kusema bado wapo kwenye mchakato, Lakini akieleza pia kuna ugumu mkubw vilabu kuachia magolikipa wao kwenye kipindi hichi cha majira ya baridi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa