Cirille Nje Kwa Wiki Sita Kisa Majeraha Ya Bega

Mlinzi wa kulia wa klabu ya Singida Black Stars kutoka mkoani Singida, Ande Kofie Cirille raia wa Ivory Coast, anatarajia kukaa nje ya uwanja kwa wiki takribani sita hadi kurejea tena kwenye uwanja kuipambania timu hiyo. Daktari wa timu amethibitisha.

Cirille alipata majeraha hayo katika mchezo wa Nusu Fainali michuano ya Mapinduzi Cup huko visiwani Zanzibar dhidi ya Yanga ambapo alisukumwa na Mlinzi wa kushoto wa Yanga Chadrack Boka na kuangukia upande wa bega hilo  kwa nguvu kiasi cha kushindwa kurejea uwanjani kuendelea na mchezo.

Cirille Nje Kwa Wiki Sita Kisa Majeraha Ya Bega

Taarifa hiyo imethibitishwa na mganga mkuu wa klabu hiyo Dkt. Shami Shonde katika mazoezi ya kwanza ya timu hiyo baada ya mashindano ya Mapinduzi yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Sheria pale Mawasiliano jijini Dar es salaam.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika maelezo yake Dkt. Shonde amesema, nyota huyo hatofanya mazoezi na wenzake kwa wiki mbili kisha atahitaji wiki nne au tatu za kufanya mazoezi na wenzake ili aweze kuimalika na kurejea dimbani.

Cirille Nje Kwa Wiki Sita Kisa Majeraha Ya Bega

Hili linaweza kuwa pigo kwa klabu ya Singida kwani staa huyo sasa atakosa michezo yote minne iliyobaki katika hatua ya makundi kombe la shirikisho Barani Afrika ambako mpaka sasa wana alama moja pekee.

Kwa hesabu nyepesi Andi Cirille atarudi dimbani mwanzoni mwa mwezi March mwaka huu na atacheza kombe la shirikisho endapo timu hiyo itafuzu kucheza Robo Fainali.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.