Kiungo mshambualiaji mpya wa klabu ya Yanga raia wa Uganda, Allan Okello, ameanza mazoezi yake ya kwanza katika klabu ya Yanga kwa ajili ya kujiandaa na michezo ijayo na mwenyewe akikiri kuwa anatamani kuanza kumwaga jasho akiwa na uzi wa mabingwa hao mara 31 Tanzania Bara.
Okello ameanza mazoezi binafasi tangu juzi akiwa jijini Dar es salaam huku akiwasubiri mabingwa hao ambao siku chache zilizopita walitwaa ubingwa wa Mapinduzi Cup huko visiwani Zanzibar, wakiwafunga Azam FC kwa penalty 5-4 baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu.
Okello alitambulishwa na Yanga Januari 12 kwa mkataba wa miaka miwili akitokea katika klabu ya Vipers ya huko nchini Uganda. Hii inaonesha Yanga wapo serous sana na hawana muda wowote wa kupoteza hasa wakikumbuka kuwa watacheza michezo miwili muhimu dhidi ya Al Ahly mwishoni mwa mwezi huu.
Bila kusahauย meridianbetย ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Okello mwenye matumizi mazuri ya mguuย wake wa kushoto amesema hana muda wa kulala na ameonekana akiwa na hamasa kubwa na ari ya hali ya juu wakati wa mazoezi, akionesha wazi kuwa yupo tayari kukabiliana na changamoto mpya ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kuipigania nafasi yake ndani ya kikosi cha Wananchi.
Ujio wake unatarajiwa kuongeza ushindani mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Wananchi, huku kocha akiamini kuwa kasi, ufundi na uwezo wake wa kufumania nyavu vitakuwa silaha muhimu kwa timu msimu huu. Okello pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, na anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliowahi kungโara katika Ligi Kuu ya Uganda pamoja na michuano ya klabu barani Afrika.