Ten Hag Amtaka Jadon Sancho kurudi Uwanjani Haraka Iwezekanavyo Kuisaidia Man Utd

Erik ten Hag anakiri Manchester United inamhitaji Jadon Sancho arejeshwe uwanjani haraka iwezekanavyo, lakini haitamlazimisha nyota huyo wa Uingereza kuharakisha kupona kwake. Pata Odds za Soka hapa.

 

Jadon Sancho

Jadon Sancho amerejea katika kambi ya klabu ya Carrington ili kufuata programu ya utimamu wa mwili, baada ya wiki kadhaa kufanya kazi peke yake nchini Uholanzi kwa sababu Ten Hag alisema hakuwa katika hali nzuri ya kimwili na kiakili kufanya mazoezi na wachezaji wengine wa kikosi hicho.

United tayari wanahitaji kusajili mshambuliaji katika dirisha la usajili la Januari baada ya kuvunja mkataba wa Cristiano Ronaldo, na Ten Hag alikiri kwamba Sancho angekuwa nyongeza muhimu kwa safu ya washambuliaji iliyopungua.

Bosi huyo wa United alifichua kwamba winga huyo mwenye umri wa miaka 22 anafanya maendeleo, lakini akasisitiza kwamba hatamsukuma Jadon Sancho kurejea kabla hajawa tayari. Unaweza kubashiri Mubashara na Meridianbet Bonyeza hapa.

“Tuna vikwazo vya kuchukua, lakini nadhani yuko katika mwelekeo mzuri,” alisema Ten Hag. ‘Nitafurahi sana wakati atakaporejea kwenye kikosi kwa ajili ya mazoezi ya timu. Hiyo ni hatua inayofuata.

“Mwili pia unaunganishwa na akili. Sasa anafanya mazoezi mazuri kwa upande wa kimwili na itamsaidia. Nadhani anaweza kurudi haraka, lakini siwezi kusema itakuwa muda gani.

“Ningependa arudi haraka iwezekanavyo. Nitafanya kila kitu katika uwezo wangu, lakini huwezi kulazimisha michakato fulani na hii ni mojawapo.

“Kwa hiyo ni lazima nionyeshe subira, ingawa sina subira kwa sababu upo sahihi, tunakosa nafasi katika mstari wa mbele. Anapokuwa fiti, Jadon Sancho ni mmoja ambaye anaweza kuchangia kisha tutakuwa na chaguo la ziada. Mechi zote Meridianbet zina Odds nono na kubwa.

“Alikuwa Uholanzi, lakini mchakato pia ungekuwa Uingereza. Nadhani wanariadha wengi bora, wakati mwingine ni vizuri kuondoka mahali ulipo kila siku ili kupata motisha na uzoefu mpya.

“Watu wana mtazamo tofauti na hii inaweza kukupa msukumo sahihi ili kurejea kwenye mstari. Wacheza kandanda sio roboti. Hakuna aliye sawa. Kwa kila mtu, unahitaji mbinu ya mtu binafsi. Tulifikiri, kwa ushirikiano na Jadon Sancho, lilikuwa chaguo bora zaidi.” Tembelea duka la kubashiri uoneshe umwamba wa kubashiri.

Acha ujumbe