Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesifu uwezo wa beki wake wa kulia Aaron Wan Bissaka kutoka na michezo kadhaa aliyocheza hivi karibuni.
Beki Aaron Wan Bissaka alipitia kipindi kigumu baada ya ujio wa kocha Ten Hag baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo, Lakini tangu kurejea kwa ligi baad ya michuano ya kombe la dunia kiwango cha beki huyo kimeimarika kwa kiwango kikubwa.
Kocha wa klabu hiyo Ten Hag ameulizwa kuhusu ubora wa beki wake huyo na kusema beki huyo amecheza vizuri katika michezo iliyopita akitengeneza uwiano mzuri kwenye kuzuia na kushambulia. Miongoni mwa matatizo makubwa ambayo beki huyo yalikua yanamsumbua basi ni kushambulia kitu ambacho anaonekana kukifanyia kazi.
Klabu kadhaa ndani ya ligi kuu ya Uingereza ziliulizia huduma ya beki huyo kuelekea dirisha dogo la mwezi Januari na vilabu hivyo ni kama West Ham,Wolves, na Crystal Palace. Lakini Ten Hag ameamua kumbakiza beki huyo ndani ya Manchester United.
Kumekua na mabadiliko makubwa kwa beki huyo tangu kurejea kwa ligi baada ya michuano ya kombe la dunia na kocha wa klabu hiyo Ten Hag alieleza mapumziko ya kombe la dunia yalimsaidia beki huyo, Sasa ni wazi kutakua na ushindani mkubwa upande wa kulia ndani ya klabu hiyo baina yake na Diogo Dalot.

