Kiungo wa klabu ya Rangers Aaron Ramsey atakosekana kwenye mchezo wa  Europa League ambao utachezwa siku ya alhamisi dhidi ya Borussia Dortmund kwenye dimba la Ibrox.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutokea nchini Wales, alijiunga na klabu ya Rangers akitokea klabu ya Juventus kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu, tokea ajiunge na klabu hiyo amefanikiwa kucheza dakika 94 tu, pia alikosekana kwenye mchezo wa wikiendi dhidi ya Dundee United ambapo walitoka sare.

Aaron Ramsey
Aaron Ramsey

Rangers kwenye mchezo wa kwanza walifanikiwa kushinda 4-2 ambapo Aaron Ramsey alikosekana kwenye mchezo huo, Giovanni van Bronckhorst alipoulizwa kuhusu uwepo wa wa Ramsey alijibu, “Aaron Ramsey hatakuwepo kwenye kikosi cha kesho lakini hakuna taarifa nyingine ya majeruhi.

“Tulikuwa na mchezo mzuri wiki iliyopita, na tunajua kuwa ule ulikuwa ni nusu ya mchezo, malengo yetu ni kucheza kwa kwa nguvu kadri iwezekanavyo ili kuweza kushinda, tulicheza kwa kujitoa ma tuliweza shambulia kwa wakati sahihi.

“Tulicheza vizuri dhidi ya Dortmund, nadhani pia tulicheza vizuri kwenye mchezo dhidi ya Dundee United lakini hatukufanikiwa kupata matokea ambayo tuliyataka.”


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa