Kocha wa As Roma raia wa kimataifa wa Ureno Jose Mourinho leo atakua akiiongoza timu hiyo kwenye fainali ya kombe la Uefa Europa League dhidi klabu ya Sevilla akilitafuta taji lake la sita la ulaya.
Jose Mourinho ameshafanikiwa kushinda mataji matano ya ulaya tofauti tofauti ambapo hili taji la Uefa Europa League ameshafanikiwa kushinda mara mbili na vilabu vya Fc Porto mwaka 2003 na Manchester United mwaka 2017, Lakini kocha huyo pia amefanikiwa kushinda taji la ligi ya mabingwa ulaya mara mbili akiwa na Fc Porto mwaka 2004, pamoja na Inter Milan 2010 na kombe la Uefa Conference mwaka jana akiwa na Roma.Kocha huyo leo atakua anatafuta rekodi kubwa ya kua kocha ambaye anakwenda kushinda fainali sita za michuano ya ulaya, Kwani Mreno huyo leo akifanikiwa kuiongoza As Roma kubeba taji hilo atakua kocha wa kwanza kushinda fainali sita kwenye michuano ya ulaya.
Jose Mourinho amefanikiwa kuirudisha Roma kwenye ubora kwani mwaka jana alifanikiwa kushinda taji la Uefa Conference League ambalo ndio ilikua msimu wake wa kwanza kuanzishwa, Lakini mwaka huu tena amefanikiwa kuiwezesha klabu hiyo kutinga fainali ya michuano ya Uefa Europa League.Kocha Jose Mourinho anaweza kufikia rekodi ya kocha wa zamani wa Sevilla ambaye kwasasa anafundisha klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza Unai Emery, Kwani kocha huyo ameshafanikiwa kutwaa taji hilo mara tatu huku Jose nae ameshinda taji hilo tayari mara mbili hivo leo anaweza kufikia rekodi ya Emery.