Kiungo wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Cameroon Franck Zambo Anguissa amefanikiwa kuongeza mkataba na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A baada ya mazungumzo kwenda sawa.
Kiungo huyo fundi ameongeza mkataba wa kuitumikia klabu hiyo mpaka mwaka mwaka 2025 huku kukiwa na kipengele cha kumuongezea kiungo huyo mkataba hadi mwaka 2027, Napoli wanashawishika kumuongezea mkataba Anguissa baada ya kuonesha ubora mkubwa klabuni hapo.Kiungo huyo wa zamani wa vilabu vya Villareal na Fulham amekua na msimu mzuri sana ndani ya klabu ya Napoli ambapo alicheza kwa mkopo kabla ya kupewa mkataba akitokea Fulham, Huku akiwa mchezaji muhimu zaidi eneo la katikati kwenye kikosi cha kocha Luciano Spaletti.
Klabu ya Napoli inaongoza ligi kuu ya Italia huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja msimu huu kitu kinachowafanya kuongeza mikataba kwa wachezaji wao muhimu ili kuendelea kuiimarisha timu yao na kuepuka kuondokewa na wachezji muhimu kitu kinachoweza kuharibu ubora wao.Kiungo Anguissa ambae pia amekua mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Cameroon ambapo anatarajia kuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachoelekea nchini Qatar kwajili ya michuano ya kombe la dunia.
Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.
BONYEZA HAPA