Kikosi cha Azam FC kimeondoka jana alhamis Jijini Dar kuelekea Morogoro kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mchezo huo utapigwa kesho Novemba 12 mwaka huu kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Akizungumza baada ya kuwasili Morogoro, Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe alisema: “Kikosi chetu kimewasili mkoani Morogoro salama kwa ajili ya mchezo wetu wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.
“Tuna jumla ya wachezaji 29 pamoja na benchi la ufundi likiongozwa na Kali Ongala pamoja na Agrey Morris.
“Morali ipo juu kwa wachezaji na leo asubuhi kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Jamhuri na tupo tayari kwa mchezo wa kesho.”