Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis Van Gaal amesema timu yake ina nafasi kubwa ya kubeba taji la kombe la dunia ambalo linatarajiwa kuanza mwezi huu tarehe 20 nchini Qatar ambapo michuano hiyo itapigwa.

Kocha huyo amezungumza hayo baada ya kutatambulisha kikosi cha wachezaji 26 watakaokwea ndege kuelekea nchini Qatar kwajili ya kupeperusha bendera ya taifa hilo kwenye michuano ya kombe la dunia.van gaalKocha Van Gaal amewaambia waandishi wa habari timu yake ina nafasi kubwa ya kubeba taji hilo na wakati akifikiria hivo vilevile wachezaji wake wanafikiria jambo hilo, kwani anaamini ana kikosi bora ambacho kinaweza kutwaa ushindani na kubeba taji  kwenye michuano hiyo.

Kocha huyo ambaye amewahi kufundisha timu hiyo kwa vipindi tofauti lakini akikumbukwa zaidi mwaka 2014 akiisaidia timu hiyo kukamata nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo iliyofanyika nchini Brazil.van gaalKocha Van Gaal ameeleza kua sio makocha wote wanaweza kusema hadharani kua timu zao zinaweza kubeba taji hilo lakini yeye amewaambia waandishi wa habari mimi sio katika wao kwani nipo hapa kuwaambia timu yangu ina uwezo wa kubeba taji la dunia.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa