Majeruhi na Kadi Zawaponza Prisons

Kocha Msaidizi wa Tanzania Prisons, Shaban Mtupa amefunguka kuwa sababu ya kupoteza mchezo dhidi ya Coastal Union ni majeruhi pamoja na kadi.

Mtupa alisema kuwa sababu kubwa ya matokeo hayo ni kutokana na idadi kubwa ya wachezaji wazoefu kuwa na matatizo mbalimbali.

“Ni kweli tumepoteza mchezo wa leo lakini tunaenda kwenye viwanja vya mazoezi kwa ajili ya kufanya baadhi ya marekebisho.

“Tuliwakosa baadhi ya wachezaji ambao walikuwa kwenye kikosi cha kwanza na hiyo ni kutokana na baadhi yao kuwa majeruhi na kadi za njano.

“Lakini hatuwezi kusema wale waliocheza hawakuwa na kiwango kizuri kwani wote ni wachezaji wetu tumewasajili na wameonyesha kiwango kizuri.”

Acha ujumbe