Klabu ya Napoli inayoshiriki ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A imeendelea kujiimarisha kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kupata ushindi leo dhidi ya klabu ya Torino.

napoliNapoli wamekua kwenye kiwango bora msimu huu baada ya kushinda michezo sita kati ya nane katika ligi kuu nchini Italia na kutokupoteza mchezo wowote katika ligi hiyo,Napoli wanakua kati ya klabu mbili pekee ambazo hazijapoteza mchezo wowote mpaka sasa hivo inaonesha kwa namna gani timu hiyo ina uwezo mzuri.

 Lucciano Spaletti anaonesha anahitaji ana ari ya kufanya makubwa katika ligi kuu ya Italia msimu baada ya kuanza vizuri katika ligi hiyo hii inatokana na namna timu yake inavyocheza inaonesha dhahiri wamejipanga kufanya makubwa zaidi.

napoliVijana wa Spaletti leo wamefanikiwa kuwafunga Torino goli tatu kwa moja katika mchezo huo mkali na kiungo Zambo Anguissa wa kalbu hiyo ameendelea kuonesha ubora wa hali ya juu msimu huu na kua miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi cha mwalimu Lucciano Spaletti.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa