Mchezaji wa zamani wa klabu ya Liverpool Martin Skrtel ameamua kutundika daluga akiwa na miaka 37 huku sababu kubwa iliyopelekea kuachana na soka ni matatizo ya kiafya baada ya kucheza soka kwa miaka 21.

Martin Skrtel alifanikiwa kuichezea klabu ya Liverpool kwa miaka nane pia aalikuwa mchezaji muhimu chini ya Rafa Benitez kwenye msimu wa 2008/09 na Brendan Rodgers kwenye msimu 2013/14 kwenye mbio za kutafuta ubingwa ambapo hawakufanikiwa na walishika nafasi ya pili.

Martin Skrtel, Martin Skrtel Astaafu Kucheza Soka Akiwa na Miaka 37, Meridianbet

Martin Skrtel akizungumza kwa uchungu kwenye kikao na waandishi wa habari alisema,  kurudi Trnava, nilitimiza ndoto yangu. nafikili kwamba hata katika umri huu bado kuna kitu naweza kuchangia kwenye timu na kuweza kucheza kwenye uwezo wangu wa juu.

“Lakini kunatatizo la kiafya. Nina tatizo la “plaques”, ambayo inanizuia sio tu kwenye soka, lakini pia kwenye maisha yangu ya kawaida. sikumbuki siku ambayo imekwisha pasipo maumivu. Nimekuwa nikifanya mazoezi  na mielekwa kwa kivuli cha dawa na sindano kwenye miezi ya hivi karibuni.

“Nimekuwa na tatizo la kutembea umbali wa mita mia na mwanangu. Maumivu ni makali sana. mbaya zaidi  nikikimbia, kuruka  na hili ndilo tunarohitaji kwenye soka.

“Kwaiyo, Nimeamua kwamba mchezo dhidi ya Dunajska uakuwa ndio mchezo wangu wa mwisho. sio tu kwa mchezo wa mwisho kwa Spartak, lakini pia kwa maisha yangu ya soka.”

Martin Skrtel mchezaji wa kimataifa wa Slovakia ameichezea klabu ya Liverpool michezo 320 kwa muda wake wote aliokaa kwenye klabu hiyo.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa