Kuelekea mashindano ya Africa Cup of Nations 2021 (Afcon 2021), timu ya Senegal imekuwa ni timu ya pili kufuzu kushiriki mashindano hayo.
Ni yuleyule nyota wa Liverpool – Saidio Mane ambaye anaendelea kuipeperusha vyema bendera ya Senegal.
Mane alifunga goli pekee kwenye mchezo dhidi ya Guinea – Bissau na kuivusha Senegal ambayo sasa ni rasmi watashiriki mashindano ya Afcon nchini Cameroon.
Senegal inashikilia nafasi ya kwanza kwa ubora barani Afrika, inakuwa ni timu ya pili kufuzu kucheza Afcon 2021 baada ya wenyeji Cameroon.
Mane ameendelea kufanya vyema akiwa na timu ya taifa, mchezo uliochezwa jumatano dhidi ya Guinea – Bissau. Mane alifunga goli 1 kwa mkwaju wa penati katika mchezo uliomalizika kwa ushidi wa 2-0.
Ushindi dhidi ya Guinea – Bissau unawapa faida Senegal wakiwa wanaongoza Kundi I kwa jumla ya pointi 12 katika michezo minne aliyocheza na wanafaida ya michezo miwili mkononi.
Mashindano ya Afcon 2021 imesogezwa mbele kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID19. Mashindano haya yataanza kutimua vumbi mwezi Januari 2022.
Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.



Carolyn
Hongera sana Senegal.Mane amewatoa kimasomaso
Lydia Emmanuel Magoti
Hongera yake Mane mpambanaji
Ester jackson
Pongezi sana mane kwa kuendeleza ushujaa wako
magdalena
safi sana mane kazi nzui umeifanya
Tahiya
Bravo
Elika
Safi sana kaka mkubwa mane,uwezo wako tumeuona
Fatina mfigi
Safi sanaa!
Rahma
Safi sana kwa kazi nzuli
Sadick
Wachezaji wengi wa Senegal huwa na utaifa hata wanapokuwa maarufu tofauti na Nigeria. Hongera Senegal
Hopemwaikuka
Congrats Sadio Mane
Angelina
Good job Mane
Mwajumah
Safi sana
Povel
Congratulations captain sadio MANE
Issa
Mane amekua mzalendo kwa nchi yak
aisha
Mane hanaga kazi mbovu safi sana kwake
Sabrina
Kazi nzuri mane
Sauda
Mane anastahili pongezi
Saupha mohamed
Hongera sana
Tatu
Sadio mane ni mchezaji mzuri