Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji amesema klabu hiyo ilishaingia mkataba mpya na kiungo Cleotus Chama.
Mo Dewji amesema mkataba wao na Chama unaisha mwaka 2022, hivyo taarifa za kuwa anakwenda Yanga zimekuwa zikiwashangaza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dewji amesema mchezaji huyo ni mali ya Simba na hakuna sababu ya kuwa na hofu.

“Taarifa sijui anakwenda Yanga ni mambo ambayo si sahihi, hakuna sababu ya kuwa na hofu na ninawatoa hofu mashabiki wa Simba kuwa tuko makini sana.
“Sehemu mbalimbali zimekuwa nikikutana na mashabiki wa Simba ambao wananiambia Mo fanya Chama asiondoke Simba. Chama ni mchezaji wa Simba.
“Suala kwamba anakwenda Yanga sijui linatoka wapi lakini haina shida, sasa nimewaambia na ninafikiri leo tunafunga mjadala,” alisema Mo Dewji.
Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.



Ester jackson
Fanya hivyo iwe kweli yasiwe maongezi pia ukumbuke kuwa ushawishi ni mzuri zaidi kuliko nguvu ya pesa inawezekana ukamshawishi na pesa lakini akakataa kudondosha saini yake kila la heri no ufanikishe hilo
Lydia Emmanuel Magoti
Maneno hayo kila mtu anaongea lake Chama bado yupo yupo simba Sana tuuu kwaio wapinzani watasubili Sana kumsubili Chama haende yanga bado Sana yani
magdalena
chama atabaki simba tu hawezi kukubali kwenda utoporo kufa njaa
Tahiya
Baelezee baba
Elika
Chama kama chama hawezi kwenda popote,hapo simba kashatua mizigo yake..najua maneno mengi yanaongelewa lakini mwamuzi ni yeye chama
Carolyn
Akae tu simba. Ata yanga hatuna shida nae.tumejitosheleza.na hamtuwezi
Fatina mfingi
Hapo umemaliza mzizi wa fitina!
Adelta
Yetu macho ngoja tuone
Rahma
Chama Kama chama atabaki kuwa simba
Hopemwaikuka
Nltaka nishangae
Angelina
Chama hawezi kwenda utopolo😀
Mwajumah
Chama awezi kuondoka simba kwan yeye na simba damdam
Povel
Chama is un stopped
Sadick
Tetesi za Chama kutaka kuondoka zinapandisha gharama yake sokoni naamini amepata mkataba mno zaidi kuliko wa awali
Issa
Chama njoo yanga upate changamoto ingine huko kwa mikia hamna. Maajabu
aisha
Aya wana simbaa kila sehemu chama duuh naona chama ndio anafunga mwaka kwa kujadiliwa
Sabrina
Hapo panamfaa tu
Sauda
Chama hawezi kuondoka Simba
Saupha mohamed
Chama atoki simba
Tatu
Yanga wanapenda kujambisha tu wajahuwezo wa kumchukua chama