Celtic ilishinda taji la Ligi Kuu ya Scottland na kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa; Rangers iliifunga PSV Eindhoven kwa jumla ya mabao 3-2 katika mechi za kufuzu; Celtic imepangwa Kundi F dhidi ya Real Madrid, RB Leipzig na Shakhtar Donetsk; Rangers kumenyana na Ajax, Liverpool na Napoli katika Kundi A.
Kipindi timu hizi zinashiriki hatua ya makundi ya UCL, Gordon Brown alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, mwaka huo ulikuwa ni ‘Ulimwengu wa ajabu sana’ ndiyo kipindi ambacho iPhone ya kwanza ilizinduliwa.
Ndiyo, Mwaka 2007 ni kama zamani sana, lakini hiyo ndiyo mara ya mwisho Celtic na Rangers walikuwa pamoja kushiriki katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa. Ingawa imekuwa na nafasi ya kipekee katika mashindano ya juu ya vilabu barani Ulaya tangu, msimu huu wote wanaweza kusherehekea kufuzu.
Rangers watamenyana na Liverpool ya Jurgen Klopp pamoja na Ajax na Napoli katika Kundi A, wakati Celtic wamepangwa dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid, pamoja na RB Leipzig na Shakhtar Donetsk katika Kundi F.
Mshambuliaji wa zamani wa Celtic Andy Walker anaamini kuwa mafanikio ya Celtic na Rangers yanaweza kuongeza wachezaji bora zaidi kuvutiwa na Ligi Kuu ya Scottland.
“Nakumbuka nilifanya kazi mara ya mwisho Celtic na Rangers zote zilipokuwa katika hatua ya makundi, moja ilicheza Jumanne na nyingine Jumatano na ilikuwa ni michezo ya kuvutia zaidi”. Alisema Andy Walker mchambuzi wa Sky Sports.