Klabu ya soka ya Real Madrid itaanza mchezo wake wa kwanza wa Spanish Super Cup dhidi ya klabu ya Valencia mchezo utakaopigwa katika dimba la King Fahd nchini Saudia Arabia.

Klabu ya Real Madrid baada ya kupoteza mchezo wake wa mwisho wea ligi kuu ya soka nchini ya Hispania dhidi ya Villarreal, Leo watajitupa dimbani kumenyana na vijana wa Gennaro Gattuso kulisaka taji la kwanza la msimu huu.Real MadridMichuano ya Spanish Super Cup ambayo inapigwa nchini Saudia Arabia ikiwa tayari ipo kwenye hatua ya Nusu fainali na klabu hiyo ikifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali, Hivo inaweza kua nafasi ya kushinda taji la kwanza msimu huu baada ya kulikosa taji hili msimu uliomalizika.

Klabu ya Real Madrid ilifanikiwa kubeba mataji mawili msimu uliomalizika ikiwemo ligi ya mabingwa ulaya na kombe la ligi kuu nchini humo La Liga, Lakini walishindwa kubeba taji hilo msimu uliomalizika na kushindwa kuweka rekodi ya kubeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja kama mahasimu wao klabu ya Barcelona.Real MadridReal Madrid wakifanikiwa kushinda mchezo wa leo dhidi ya Valencia watakua wamefuzu hatua ya fainali ya michuano ya Spanish Super Cup, Lakini klabu ya Barcelona inacheza kesho dhidi ya bingwa mtetezi klabu ya Real Betis hivo Barca wakishinda ni wazi kua klabu Spanish Super Cup itazalisha mechi ya EL Clasico nchini Saudia Arabia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa