Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez ameonekana kuwahofia waandishi wa habari endapo klabu yake haitafanikiwa kubeba taji lolote msimu huu.
Kocha huyo ambaye kwasasa yupo na klabu yake ya Barcelona nchini Saudia Arabia ambapo ndipo michuano ya Spanish Super Cup itakapofanyika mwaka huu. Xavi amemueleza waandishi leo kua yupo klabuni hapo kwajili ya kushinda mataji na hivo kama akishindwa kubeba taji anasema anajua waandishi watamuua.Klabu ya Barcelna inaongoza ligi kuu ya soka nchini Hispania ikiwa juu kwa alama tatu zaidi ya mabingwa watetezi klabu ya Real Madrid ambao walipoteza mchezo wao dhidi ya klabu ya Villarreal wikiendi iliyomalizika na kuifanya Barca kuongoza kwa alama tatu.
Kocha huyo ambaye kesho ataenda kucheza mchezo wake wa kwanza wa Spanish Super Cup dhidi ya mabingwa watetezi klabu ya Real Betis, Huku Xavi akiendelea kusisitiza wameenda kupambana ili waweze kubeba taji hilo lakini pia ameelza fika kua Real Betis ni wapinzani wagumu hivo mchezo utakua mgumu.Kocha huyo Xavi Hernandez amesema anajua umuhimu wa kushinda taji la Spanish Super Cup ambapo mchezo wa fainali utapigwa siku ya jumapili kwani kushinda taji hilo kutawapa utulivu wa akili, Lakini pia endapo hawatashinda hatabadilisha sana mambo na mipango yao ambayo wamejiwekea msimu huu.