Ronald Koeman Afungashiwa Virago na Barcelona

Ronald Koeman amefungashiwa virago na waajiri wake Barcelona baada ya kupokea kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Rayo Vallecano kwenye dimba la Campo de Futbol de Vallecas.

koeman amedumu Barcelona kwa miezi 14, huku akiingoza Barcelona kwenye michezo 67 akishinda michezo 39, katoa sare michezo 12 na kupoteza michezo 16 pia alifanikiwa kuwaongoza barcelona kuweza shinda taji la copa del rey baada ya kuifunga timu ya Athletic Bilbao goli 4-0 kwenye mchezo wa fainali.

koeman
Ronald Koeman

Raisi wa Barcelona Joan Laporta alitoa taarifa hiyo baada ya kipigo cha Rayo Vallecano alisema, “Ronald Koeman ataaga timu leo alhamisi kwenye viunga vya Ciutat Esportiva, tunashukuru kwa huduma yake kwenye klabu na tunamtakia maisha mema kwenye kazi yake.”

Barcelona wako nafasi ya tisa wakiwa na pointi 15 kwenye michezo 10 kwenye ligi kuu ya Hispania La Liga.

Ronald Koeman

Kulingana na tetesi zilizopo mchezaji wa zamani wa Barcelona aliyecheza kwa mafanikio makubwa, kiungo aliyekuwa nyota wa timu Xavi Hernandez anapigiwa chapuo la kubeba mikoba ya Koeman kwenye klabu hiyo


MCHONGO WA PESA NA CIRCUS FEVER

Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe