Mgombea urais wa Barcelona Victor Font anataka kumrudisha Pep Guardiola kutoka Manchester City.
Josep Maria Bartomeu tayari alishatangaza kujiuzulu kama rais huko Camp Nou Jumanne, yakiwa ni maamuzi ya kukwepa kura ya kutokuwa na imani dhidi ya uongozi wake, akijumuishwa pamoja na bodi nzima ya wakurugenzi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari Hispania, kufuatia uamuzi wa Bartomeu kujiuzulu, uchaguzi wa urais wa Barcelona mpya utafanyika wiki ya pili ya Januari, na Font akitajwa kuwa mmoja wa wanaotaka kuwania nafasi hiyo.
Font, mwenye miaka 48, alidai kwamba ikiwa atachaguliwa kuwa raisi, atafanya kila awezalo kumrudisha Guardiola kama mkufunzi mkuu. Pia raisi alisema anataka kuhakikisha Messi anasalia Barcelona.
Guardiola alipata mafanikio kwa nafasi yake alipoiongoza Barcelona kati ya 2008 na 2012, alitwaa LaLiga mara tatu na kombe la Ligi ya Mabingwa mara mbili.

Messi, wakati huo huo, tayari alikuwa ameonyesha nia ya kutaka kuondoka Barca mnamo Agosti, lakini kutokana na mgogoro wa mkataba wake alilazimika kuamua kusalia huku mkataba wake ukikamilika mwishoni mwa msimu wa 2020-21.
Mpango alionao mgombea Victor Font, ni kuhakikisha anaweza kuirejesha huduma ya Pep Guardiola. Anaamini Guardiola anaweza kuirejeshea heshima klabu hiyo.
Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.
Kamata Mkwanja wako HAPA


Sabrina
Victor akifanikiwa kumrudisha guardiola itakua poa sana
Elika
Guarduola angerudi tu
warda
Itakuwa poa sana kumrejesha Guardiola
Ernest
Itakuwa Ngumu sana kwa Pep kurudi Barca
Dorophina
Man City sidhani kama watakubali kumuachia guardiola haende barca
zeiyana
utakua hujio mzuri kwa barcelona kama victoria hatasalia clabuni hapo
Adelta
Hapo sithani Kama atarudi Barcelona
Khadija
Kurudi hapo sidhani
Sauda
Afadhali Guardiola arudi
Lydia Emmanuel Magoti
Itakuwa vizuri akifanyikiwa kumludisha kocha huyo Guardiola
Carolyn
Duuh sidhani ni Kama ni rahisi kiivo
Tatu
Guardiola ni kocha anayeiweza barcelona
Mwajumah
Bora tu Guardiola alud maana ni kocha mzuri sana
Hopemwaikuka
Itakua vzur tu
Issa
Guadiola atawez kuirudisha barca enzi zake
Povel
Kila la kheri
Saupha mohamed
Kila la kheri
Fatuma kasomo
Kila la heri