Klabu ya Barcelona hatimaye wamekaubali kiasi cha €65milioni kutoka klabu ya Manchester United ili kumuuza kiungo wake wa kiholanzi Frenkie de Jong, ijapokuwa bado kuna mazungumzo yanayoendelea lakini ada ya uhamisho sio tatizo tena.

Barcelona na Man Utd bado wapo kwenye mazungumzo ya msingi kuhusu uhamisho wa De Jong, ambapo kwenye kiasi cha €65milioni kinaweza kuongezeka kufikia hadi €80milioni.

Barcelona

Mwandishi wa kimataifa anayehusika na habari za usajiri Fabrizio Romano, anaamini kuwa uhamisho huo unaweza kuwa €85milioni, katika maongezi ambayo yanayotarajiwa kuendelea wiki hii, ada ya uhamisho inaweza kuongezeka hadi kufikia  €100milion, kiasi ambacho klabu ya Barcelona wanahitaji.

Mpaka sasa kuna mwanga mkubwa kwenye uhamisho wa muholanzi huyo kuachana na Barcelona kwenda Man Utd.

Kabla kwenda kwenye mapumziko wiki mbili zilizopita, Frenkie de Jong wakati akihojiwa alisema kuwa bado anafuraha kubakia Barcelona.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa