Gérald Darmanin Aomba Radhi kwa Usimamizi M'bovu wa Mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Waziri wa mambo ya ndani Gérald Darmanin ameomba radhi kwa wale wote waliopata shida kwenye mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa mpangilio m’bovu ambao ulipelekea mashabiki kushambuliana na polisi kwenye uwanja wa Stade de France jijini Paris.

Awali, Gérald Darmanin aliwalaumu mashabiki wa Liverpool kwa kufanya fujo, ambapo wengi wao walikuwa na idadi kubwa ya tiketi za bandia kwenye uwanja wa Stade de France na kusababisha vurugu kupelekea polisi kutumia vipulizi vya kuwasha na mabomu ya machozi.

Gérald Darmanin

Gérald Darmanin wakati akiwa anafanyiwa mahojiano na kituo cha radio RTL alinukuliwa, “je nilikuwa sehemu ya watu wanaopaswa kuwajibika? jibu ni ndio bila shaka, niko tayari kuomba radhi kwa kila mmoja ambaye alidhurika kutokana na mpangilio m’bovu wa mchezo ule.”

Pia alisema alijifunza kitu kutokana na tukio lile, ndio maana Ufaransa ilipokuwa mwenyeji wa michezo miwili ya kimataifa ya fainali ya Top 14 rugby kwenye uwanja ule ule hakukuwa tena tatizo kubwa kama kwenye mchezo wa fainali ya UEFA.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

Acha ujumbe