Mchezaji nyota wa klabu ya Barcelona Ousmane Dembele ambaye mkataba wake unakwenda kusha baada ya mwezi anapigiwa upatu kujiunga na klabu ya chelsea ili kuunga na kocha wake  Thomas Tuchel ambaye alicheza kwa mafanikio akiwa chini yake.

Ousmane Dembele amekuwa hana misimu mizuri kwenye klabu ya Barcelona tokea ajiunge na klabu hiyo akitokea klabu ya Dortmund, huku muda mwingi akitumia kujiuguza majera mara nyingi kuliko muda anaotumia akiwa uwanjani lakini chini kocha mpya Xavi ameonekana kuwa ni moja ya wachezaji ambao anataka kumbakisha kwenye klabu hiyo.

Wakati klabu ya Barcelona wakianda mkataba mpya kwa ajiri ya kumpatia mchezaji huyo, kuna tetesi zimemezuka kuwa Dembele tayari kashafanya makubaliano na klabu ya Chelsea na tayari ameshasaini mkataba na klabu hiyo.

Mwanahabari wa kuaminika wa kiitariano ambaye anaripoti habari za usajiri, Fabrizo Romano, kwenye ukarasa wake wa twitter alitoa taarifa na kuthibitisha kuwa Dembele tayari kashamwaga wino kwenye klabu ya Chelsea na amelamba mkataba wa miaka minne ambao unatarajia kumalizika June 2026.

Ousmane Dembele atajiunga na klabu tajiri ya London ‘The Blues’ mapema July kwenye majira ya kiangazi kwa uhamisho huru.


Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.

Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa