Ousmane Dembele anajiandaa kuachana na klabu ya Barcelona kwenye uhamisho huru baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitano japo muda mwingi amekuwa nje ya uwanja akiugaza majeraha huku akikosa michezo muhimu kwenye klabu hiyo.

Ousmane Dembele hivi karibuni amekuwa akihusishwa zaidi na kujiunga na klabu ya Chelsea, kufuatia kukataa mikataba kadhaa ambayo klabu ya Barcelona imekuwa ikimuandalia ya kutaka kumbakisha kwenye klabu hiyo.

Ousmane Dembele

Dembele alijiunga na klabu ya Barcelona mwaka 2017 akitokea klabu ya Borussia Dortmund kwa uhamisho ulioigharimu £120million, lakini tokea asajiriwe amekosa michezo zaidi ya 100 kutokana na majeruhi ya mara kwa mara ambayo yamemfanya asiwe na wakati mzuri kwenye klabu hiyo.

Tokea Xavi achakue hatamu kuingoza klabu ya Barcelona, amejaribu kufufua matumaini ya Ousmane Dembele ambapo chini yake amefanikiwa kuanza michezo 18, na kufunga goli moja tu, lakini kinachovutia kuwa katoa pasi za mwisho 13, ikiwa ni mchezaji aliyetoa pasi nyingi za magori tokea mwaka huu uanze barani ulaya.

Xavi alielezea shauku yake ya kutaka kuendelea kufanya nae kazi mwezi November mwaka jana.

“Kumuongezea mkataba Ousmane Dembele ni moja ya kipaumbele chetu. Ndio, anaweza kuwa moja ya wachezaji bora kwa nafasi yake. 

“Ousmane inabidi afanye kazi sana, anakitu anachoweza ifanya Barcelona ikawa tofauti kama mchezaji bora. Lakini anahitaji muendelezo mzuri.”


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa