Klabu ya Barcelona baada ya miezi kadhaa ya sintofahamu na kutupiana maneno kuhusu kumsainisha mkataba mpya mchezaji wake Ousmane Dembele sasa mwangaza umeanza kuonekana baada ya kufungua milango ya mazungumzo.

Kocha wa klabu hiyo Xavi Hernandez na raisi Laporta, wamekuwa wakizungumza mara kwa mara kuhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, kuna kipindi ilifika mpaka wakawa wanapishana huku raisi anatoa kauli hii, kocha anatoa kauli hii.

Barcelona

Kwa taarifa zilizotufikia mpaka sasa ni kuwa mkurugenzi wa michezo klabu ya Barcelona Mateu Alemany amewasili jijini Marrakech kufungua milango ya maongezi kuhusu mkataba mpya na wakala wa Dembele Moussa Sissoko.

Moussa Sissoko yuko nchini Morrocco kwa shughuri za kibiashara, ambapo mchezaji huyo wa kimataifa wa ufaransa amemuomba kumpokea Alemany na msafara wake wa Barcelona kwa ajiri ya kufanya kikao.

Ikiwa Dembele atakubali kumwaga wino kwenye klabu ya Barcelona, basi atakuwa ameipunguzia klabu hiyo gharama kubwa ya pesa ambayo alikuwa anapata na kuipa shida klabu kutafuta mchezaji wa kuweza kuziba nafasi yake kwenye majira ya kiangazi.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa