Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola kwenye kikao na waandishi wa habari kabla ya mchezo wake wa kwanza na klabu ya Atletico Madrid alisistiza kuwa anafikilia zaidi ili kumsaidia kuwa na mbinu nyingi zaidi ili kutokucheza kwa mfumo moja mara zote.
Pep Guardiola kesho anamkaribisha Diego Simeone kwenye dimba la Etihad Stadium kwenye mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya, huku kocha huyo wa klabu ya man City akiwaacha watu na maswali pale aliposema kuwa anakwenda kutumia mbinu mpya.
“Mara zote natengeneza mbinu mpya na mawazo mapya, na kesho mtaona mbinu mpya,” Pep Guardiola.
“Mara zote nimekuwa nikifikilia sana, ndio maana nimekuwa na matokeo mazuri kwenye ligi ya mabingwa ulaya, napenda kazi, itakuwa haina motisha ikiwa kila siku nikifikilia vile vile tu, ikiwa watu watafikilia kuwa nitacheza sawa kati ya Liverpool na Atl Madrid, sifikili hivyo, kwa sababu jinsi wanavyocheza liverpool ni tofauti kabisa na Atl Madrid.
“Ndio maana napenda kufikilia zaidi, na kutengeza mbinu za kijinga, na kama hatushinda naadhibiwa. Kesho nitakuwa nachukua hamasa na nakwenda kucheza na mbinu za ajabu kesho. Tutacheza na wachezaji 12 kesho,” aliongezea kwa utani.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.