Xavi ameshindwa kuzungumzia hatma ya nyota Frenkie de Jong. Klabu ya Barcelona ilitajwa kuwa na mpango wa kumuuza nyota wao De Jong, ili kupunguza mzigo wa kifedha ambao klabu inao kwa sasa.

Hata hivyo, bosi huyu ameshindwa kubainisha mpango wa wazi wa Barcelona juu ya hatma ya staa wao.

Xavi amenukuliwa akisisitiza umuhimu wa nyota huyu kwenye kikosi chake, licha ya kushindwa kutaja kuwa bado klabu imeshikilia msimamo wa kumuuza Frenkie de Jong.

Kwa mujibu wa Sport, nukuu ya Xavi inaonesha kuwa klabu bado inafanya tathimini ya hali ya kiuchumi na uwezekano wa kufanya maamuzi kadhaa, ikiwa ni pamoja na hatma ya nyota huyu.

“kwangu ni mchezaji muhimu sana. Amekuwa akianza karibu kila wakati. Ni mchezaji muhimu lakini bado kuna suala la kiuchumi ambalo tunapaswa kulitazama”

 

“Tunahitaji kujua hali ya kiuchumi ili tuweze kufanya maamuzi fulani na tutafanya maamuzi moja baada ya jingine. Ni mchezaji ambaye nampenda sana, lakini tutatazama haki itakuwaje.”

 

Xavi Hernandez

Frankie De Jong Barcelona Xavi
Frankie de Jong

Kwa mujibu wa Gerard Romero, kupitia Goal, Manchester United ni moja ya klabu ambayo inatajwa kuwa karibu kuipata saini ya Frenkie de Jong, ikiwa Barcelona wataamua kumuuza nyota huyu.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa