Klabu ya Newcastle United imefikiana makubaliano na klabu ya Aston Villa kwa mchezaji wake Matt Targett ambaye alikuwa anaichezea klabu hiyo kwa mkopo wa muda mfupi ambapo alijiunga na  Magpies mwezi january.

Matt Targett amefanikiwa kukichezea kikosi cha Newcastle United michezo 16 tu, pia ameisadia klabu hiyo kuoka kwenye hatari ya kushuka daraja na kufanikiwa kushika nafasi ya 11 kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Newcastle United

Wakati klabu ya Newcastle United inamsajiri kwa mkopo wa muda mfupi walipewa kifungu cha kuweza kumnunua moja kwa moja kwa ada ya uhamisho inayofikia £15million, ukiondoa ada ya uhamisho wa mkopo iliyolipwa mwezi January.


Kufuatiwa na kuwasiri kwa mkurugenzi mpya wa michezo Dan Ashworth wiki hii, Klabu ya Newcastle United amekamilisha usajiri wake wa kwanza ambao anakwenda kulipa kiasi cha £12million kwa klabu ya Aston Villa.

Matt Targett alikamilisha vipimo vyake vya afya siku ya jumatano na kuhakikisha anafanikisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu hiyo ya Magpies.


Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.

Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa