Lyon imethibitisha kurejea kwa mshambuliaji Alexandre Lacazette kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kuondoka kwake Arsenal.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ataondoka rasmi kwa Washika Mtutu mwishoni mwa mwezi baada ya kuwepo kwa miaka mitano Kaskazini mwa London.

Lacazette aliwahi kuwa kwenye kikosi cha vijana cha Lyon msimu wa joto wa 2003 akitokea akademi na kuichezea klabu hiyo mara 275 kwenye mashindano yote.

Mfaransa huyo alifunga mabao 129 na kutoa asisti 43 kwa Lyon katika kipindi cha miaka nane kwenye kikosi cha kwanza na alimaliza kama mfungaji bora wa msimu wa 2014-15 wa Ligue 1 akiwa na mabao 27.

Lacazette alishinda taji moja la Coupe de France na Trophee des Champions mara mbili kabla ya kuhamia Arsenal kwa pauni milioni 47.7 msimu wa joto wa 2017, akifunga mabao 17 katika msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo.

“Tumamua kuachana na klabu na mimi kufuata uelekeo mpya baada ya kumalizika kwa mkataba wangu. Huu ni wakati wangu wa kupata uzoefu mpya na kufurahia mazingira mapya.” – Alexandre Lacazatte

alexandre lacazette to lyon

Staa huyu anasema kuwa anafurahia kwamba alipata nafasi ya kuichezea klabu ya ndoto zake, aliyotamani kuichezea akiwa mdogo.

Lacazatte anaondoka na kumbukumbu ya magoli 71 na asistu 36 katika mechi zake 206 alizoichezea klabu ya Arsenal kati ya mwaka 2017 na 2022. Mkataba wake wa sasa na Lyon utadumu hadi mwaka 2025.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa. Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa